Jiji
letu la Dar es Salaam limepata heshima ya kimataifa, katika nchi ya
Ujerumani kwenye Jiji la Hamburg, Kuna sehemu imepewa jina la Dar Es
Salaam Platz ( Dar es Salaam square ).
Kutoka
kulia : Brighton Monyo ( Zimamoto DSM ), Bw. Wilson M. Kabwe (
Mkurugenzi wa Jiji DSM ), Mh. Christopher H. Mvula ( Kaimu Balozi wa
Tanzania nchini Ujerumani ), Godwin D. Msigwa, Bw. Ali Siwa, Bw. Philip
H. Mwakyusa wakati wa Uzinduzi wa Viunga vilivyopewa jina la Dar Es Salaam.
Mh.
Dr. Didas Masaburi ( Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ) akipata
maelezo kutoka kwa wenyeji wa Jiji la Hamburg akiwa katika sehemu ya Dar
es Salaam.
Kutoka
kulia : Moses Haule, Godwin Msigwa, Ully Mbuluko, Godfrey Matola na
Brighton Monyo ( Watanzania waliopelekwa kwa Mafunzo mjini Hamburg )
wakiwa chini ya kibao kinachoonyesha ile sehemu ya Dar es Salaam jijini
Hamburg.
Huo
ndio muenekano wa sehemu ( Dar es Salaam square ) Jijini Hamburg, hapo
kuna viunga na kivuli ambapo watu mbali mbali wakati wa tofauti hufika
na kupumzika, kusoma vitabu, kukutana na marafiki nk.
Viongozi
wa Tanzania wakiwa chini ya kivuli wakati wakisubiri ufuguzi hafla ya
ufunguzi wa viunga vya sehemu ya Dar es Salaam Platz ( Dar es Salaam
Square ).
No comments:
Post a Comment