Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Vijana wamachinga wa Mwenge DSM leo wamegeuka na kuwa Polisi. Kilisikika kipaaza sauti kutoka katika gari la matangazo leo asubuhi. Katika kutafuta mahali pa kukimbilia kujificha niliona wamachinga hao vijana wa kike na kiume wakiwa na vifaa maalum mikononi kama mafagio, reki, gloves mikononi na mifuko mikubwa ya rambo. Hapo ndipo nilipata ujasiri wa kusogea karibu na kuwakuta vijana hao wakifanya usafi maeneo yote yanayozunguka Mwenge kituoni na vitongoji vya karibu. Usafi huo uliambatana na hamasa kutoka katika gari la matangazo lililokuwa likitembea pamoja na wamachinga hao huku likitoa muziki mzito wa kisasa na wamachinga hao wakiendelea kufanya usafi kwa stail ya kucheza muziki. Katika kipindi kifupi sana, maeneo yote ya Mwenge yalikuwa masafi kama Kigali na Moshi Hakuna karatasi, mchanga, vumbi, rambo, magunzi, vocha, chupa..... vilivyokuwa vinaonekana tena. Nilipomuuliza mmoja wao ni kwa nini wamejiita polisi akanijibu kuwa kuanzia sasa wao ni "POLISI WA MAZINGIRA"
Kwamba kuanzia sasa wamachinga na wafanya biashara wote wa maeneo ya Mwenge watakuwa wanafanya u.safi katika maeneo ya mwenge kila siku ya Jumamosi na kuwa hakuna mtu ataruhusiwa kutupa takataka hovyo katika viunga vya Mwenge. Hii ni changamoto kwa serikli ya hapa kuhakikisha kuwa ari hii inaendelea na kujifunza kuwa sio kila wakati wamachinga ni wafanya fujo. Ni watu wastaarabu na wanaweza kufanya mambo makubwa kama wakiunganisha kwa kuhamasishwa. Ni matumaini yetu kuwa hata ile miradi ya majalala inayotuzunguka maeneo ya Mwenge yatatafutiwa maeneo maalum na si karibu na makazi ya watu au biashara.
Tahadhari kwa wapitaji wa Maeneo ya Mwenge "USITUPE TAKATAKA HOVYO KATIKA ENEO HILI MAANA UKINASWA NA POLISI WA MAZINGIRA UTAWAJIBISHWA.
Picha mbali mbali zikionyesha polisi wa mazingira wakifanya usafi katika Viunga vya Mwenge
No comments:
Post a Comment