Wachezaji wa Young Africans wakisherehekea Ubingwa wa kombe la
Kagame 2012 baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika mchezo wa fainali
Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame kwa miaka miwili
mfululizo timu ya Young Africans hawatashiriki tena mashindano ya Vilabu Bingwa
Afrika Mashariki Kati (CECAFA Kagame Cup) yaliyopangwa kuanza kutimua
vumbi nchini Sudan wiki ijayo Juni 18 siku ya jumanne.
Young Africans haitashiriki mashindano hayo kufuatia kauli ya
serikali ya juu ya kutozirushu timu zake kwenda kwenye mashindano hayo kutokana
na hofu ya usalama kwa wachezaji na viongozi wakati wa mashindano hayo.
Mapema jana Bungeni Naibu Waziri wa michezo na Utamaduni mh Amos
Makalla alisema hali ya usalama katika miji ya El- Fashir na Kadugli sio nzuri,
hivyo wao kama serikali hawataziruhusu timu za kutoka Tanzania kwenda kushiriki
michuano hiyo kutokana na hali ya usalama kwenye majimbo hayo."Sehemu
ambayo mashindano yanafanyika hakuna usalama wa kutosha, mwisho kutembea saa 12
jioni, huduma za hoteli ni duni hazijitoshelezi kuweza kukaa kwa timu katika
miji hiyo na kubwa zaidi ni hali ya usalama, kutoka Khartoum mpaka Al Fashir inabidi
kutumia usafiri wa Helikopta kitu ambacho bado ni hatari" alisema
Makalla"Kufuatia kauli hiyo ya waziri mwenye dhamana ya michezo timu ya
Yanga haitashiriki mashindano hayo, Yanga inajiondoa kwenye mashindano hayo
moja kwa moja kufuatia kauli hiyo ya serikali ya kuzizuia timu za Tanzania
kutoshiriki michuani hiyo kutokana na hofu ya usalama kwa raia wake.Kocha mkuu
Brandts mara baada ya taarifa hiyo ya serikali amesema ni jambo la busara,
serikali imetazama mbali na kuona umuhimu wa usalama kwa watu wake, kwani
hamuwezi kucheza michuano zaidi wa wiki mbili katika maeneo yanayolindwa na
vikosi vya jeshi vya kutuliza amani kutoka sehemu mbali mbali.Yanga iliyokua
imeanza mazoezi wiki iliyopita kujiandaa na mashindano hayo, kwa sasa itakua na
mapumziko ya wiki mbili kabla ya kuanza tena mazoezi ya maandalizi ya msimu
mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment