Chatu mkubwa
Chatu ana uwezo wa kumeza mnyama mkubwa kama nyumbu na hata mamba.
Kelvin akiwa hospitalini baada ya kuokolewa na wenzake
Raia mmoja mkazi wa Mwinilunga nchini Zambia ameponea chupu chupu kufa baada ya kuvamiwa na chatu.
Kelvin Katoka ambaye ni dereva wa malori yanayochimba mchanga katika machimbo ya Copa alirukiwa na chatu huyo mkubwa na kuanza kumzungurusha kwa nia ya kuanza kummeza mzima mzima.
Hata hivyo, Kelvin alipambana na chatu yule kwa kumng'ata sehemu mbali mbali za mwili wa ke bila mafanikio. Hapo Kelvina mwenye umri wa miaka 25 tu alijitahidi kuchomoa kisu mfukoni na kumchoma joka huyo mara kadhaa kabla hajaishiwa nguvu na kupoteza fahamu wakati ambapo bado chatu yuke alikuwa ameshinda na kumminya na kuanza kummeza.
Kelvin akishahis mate ya nyoka yulekichwani ndipo wafanyakazi wenzake wawili walipopita katika eneo lile na kumuua nyoka yule na kumkimbiza Kelvin Hospitalini. Kelvin anaendelea vizuri na matibabu.
No comments:
Post a Comment