Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC.
Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili juzi uwanja wa ndege wa Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika
akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza
anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery
Tesha
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM
Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe.
Lowassa
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye
mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe.
Lowassa
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara
akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege juzi
Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh
Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani
hapo kumpokea.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwa ameambatana
na makada wa chama, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini
Mwanza, wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwaajili ya mkutano wa muda mfupi
ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga wa
jijini hapa.
Alipowasili alikaribishwa kishupavu na
vijana.
Kisha akapanda mti eneo hilo ikiwa ni ishara ya
kuthamini mazingira.
Naye diwani wa Nyamagana Bhiku Kotecha alifungua
mkutano huo kwa maneno machache.
Lowassa akiwapa somo wamachinga
Mwanza.
Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20
Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara
wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya
Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga
makofi).
Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya
shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya
kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye
risala.
Mhe. Lowassa akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji
wadogo kuliko wote wa timu ya Machinga Fc inayoshiriki ligi ya kuwania kombe la
Meya's Cup jijini Mwanza
Sehemu ya umati wa wamachinga ukishangilia Maneno
yaliyowagusa kutoka kwa lowassa:-
“Ninyi ni watanzania wenye
kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu
mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote
hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili
kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza na kujiingizia kipato katika biashara
zenu za ujasiliamali”alisema.
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa akizungumza na
wananchi waliojitokeza katika hafla ya Harambee iliyofanyika katika Hotel Gold
Crest jijini Mwanza, kuwahamasisha kutambua nini wanapaswa kufanya ili
kufanikisha lengo lililokusudiwa.
WAZIRI Mkuu mstaafa
Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya
kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa
wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini
Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na
marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi
na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya
jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao
hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi
milioni 590 zikiwemo ahadi.
Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza ambaye pia ni Mzee
wa baraza la wazee Mwanza Mjumbe wa NEC wilaya ya Tarime Mhe. Christopher
Gachuma akimkabidhi mmoja wa wazee wa kiislamu aliyeketimeza kuu kanzu pamoja na
joho kama zawadi aliyovikwa mgeni rasmi Mhe.
Lowassa.
Lilikuwa tukio la kipekee Mhe. Lowassa alivikwa na
kukabidhiwa zawadi ya kibarakashia
juu..
"Ninaamini vituo vya redio
Iqra FM na redio Sauti ya Qur-ani kitaonyesha Uislamu kama dira unayohusisha
mambo yahusuyo jamii. Ni cheche ya kimungu ambayo inatoa ubinafsi pia inayo
waunganisha binadamu katika jamii moja. Korani inasema binadamu ameumbwa
kutokana na roho moja, kama mwanaume na mwanamke, jamii na mataifa, ili watu
waweze kufahamiana. Inawaleta watu wa imani zote kwenye jukwaa moja, kwa kupitia
wema.''
Pesa mbalimbali zikihesabiwa kwenye harambee iliyoongozwa na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli Edward lowassa ya
kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa
wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini
Mwanza.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli Edward lowassa akiondoka baaada ya kuongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya
kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa
wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini
Mwanza.Picha Zote na Habari na Mdau Albert G.
Sengo-Mwanza
No comments:
Post a Comment