ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, July 26, 2013

Mambo yameanza kumwendea vizuri Edward Snowden Nchini Urusi



Serikali ya Urusi imetoa nyaraka kwa Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi nchini Marekani CIA Edward Snowden zinazomruhusu kuondoka katika eneo la Uwanja Ndege ambalo amekuwa akiishi tangu awasili akitoke China. Shirika la Habari la Umma la Urusi RIA limethibitisha kupatiwa kwa nyaraka hizo kwa Snowden ambaye amekuwa akihaha kuomba hifadhi kipindi hiki akisakwa kwa udi na uvumba na Serikali ya Marekani baada ya kuvujisha siri za Shirika la CIA. Nyaraka hizo zimetoa nafasi kwa Snowden kuweza kuingia nchini Urusi na kuomba hifadhi au hata kuondoka na kueleka katika nchi yoyote ambayo itakuwa tayari kumhifadhi bila ya walinzi wa mpaka kumzuia. Taarifa zinasema baada ya Snowden kupatiwa nyaraka hizo muhimu anatazamia wakati wowote ataondoka katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Moscow alipokuwa anahifadhiwa sehemu ya abiria wanaopita nchi hiyo kueleka mataifa mengine.
Snowden amepata nyaraka hizo muhimu kutoka kwa usaidizi wa Mwanasheria wake Anatoly Kucherena ambaye amekwenda katika Uwanja wa Ndega wa Sheremetyevo kukutana na mteja wake. Nyaraka hizo amekabidhiwa Kucherena ambaye ndiye atamkabidhi Snowden anayetajwa tayari ameshabadilishiwa hadi mavazi yake tayari kwa kuingia nchini Urusi na kuendelea na mchakato wa kuomba hifadhi ya kudumu. Mwanasheria wa Snowden, Kucherena amesema iwapo mteja wake atakuwa tayari kupatiwa uraia wa Urusi atafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo ambayo huenda ikatolewa kwake bila pingamizi.
Mapema mwezi huu Snowden alijitokeza na kuomba hifadhi nchini Urusi ambapo aliambiwa mchakato wa yeye kupewa hadhi huyo huenda ungechukua hata kipindi cha miezi mitatu kabla ya kukubaliwa. Mfanyakazi huyo wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Nchini Marekani CIA Edward Snowden amekuwa akipata hifadhi ya muda nchini Urusi kitu ambacho kimechangia kuleta mgogoro wa uhusiano baina ya Serikali za Washington na Moscow.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...