Dj
Luke akiambatana na mgeni wake Mhe. Ali Hassan Mwinyi kuelekea ukumbini
kulikofanyika Tamasha la Utamaduni wa kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya
Vijimambo Jumamosi July 6, 2013 na kuwa tamasha la kihistoria
lililohudhuriwa na Watanzania wakiwemo wadau wanaozungumuza Kiswahili
wapatao 600 kutoka kila kona hapa Marekani, Ulaya na Tanzania.
Kutoka
kushoto ni Dj Luke, Mhe, Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Ramadhan Muombwa
Mwinyi, Mama Lily Munanka, Idd Sandaly na Baraka Daudi katika picha ya
pamoja wakati wakiingia ukumbini.
Watoto wa darasa la Kiswahili DMV wakiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiongea machache kabla ya kumkaribisha Dj Luke.
Dj Luke akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akishukuru kamati ya maandalizi na kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Rais
Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya Watanzania waliofika
kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya
Vijimambo na kulifungua rasmi.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Haji akisoma shairi alilotunga
maalum kwa ajili ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la
Utamaduni wa kiswahili Marekani.
Shilole
na Masanja mkandamizaji wakikandamiza na kugaragaza kwenye Tamasha la
Utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.
Shilole(mwenye
gauni la punda milia) akimnyanyua Afisa Ubalozi Mindi Kasiga kwenye
moja ya nyimbo zake alizotumbuiza kwenye tamasha hilo.
Mhe.
Ali Hassan Mwnyi akiaga na kuelekea kwenye gari lililomleta tayari kwa
kuondoka baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya tamasha hilo na sherehe
ya miaka 3 ya Vijimambo.
Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa tayari kuondoka.
kwa picha zaidi bofya read more.
No comments:
Post a Comment