ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, July 2, 2013

MHUBIRI RAIA WA UGANDA AKAMATWA NA POLISI IRINGA KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU


 

 Mhubiri Raia  wa Uganda Richard Mwangusi akiwa  chini ya  ulinzi wa  polisi  usiku  huu baada  ya kutuhumiwa kujipatia  fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia huduma ya M-PESA  

 Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa (RPC) Ramadhan Mungi akitoa  kituo  cha  polisi mjini Iringa ambako mhubiri  huyu anashikiliwa na  jeshi la polisi kufuatia wananchi kulalamika kufanyiwa  vitendo vya kitapeli na mhubiri  huyo ,kamanda  Mungi amekuwa ni mmoja kati ya makamanda wa mfano  nchini kutoka na kufanya kazi usiku na mchana na kuwa  jirani  zaidi na askari  wake 
 Kikosi  cha kazi  cha  jeshi la polisi  mkoa  wa Iringa  wakiwa njeya  kituo  cha  polisi ambako mhubiri  huyo anashikiliwa usiku  huu kwa  tuhuma za kujipatia  fedha  kwa njia ya udanganyifu 

.....................................................................................................................................................

KILIO  cha  wengi kuhusiana na vitendo vya utapeli  vinavyofanywa na baadhi ya  wahubiri ambao  wamekuwa  wakijitafutia  fedha  kupitia  injili hapa nchini ,kimeanza kusikilizwa  baada ya  jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  kumkamata  na kumtupa mahabusu  mhubiri  Richard Mwangusi ambae ni raia  wa nchini uganda   kwa  tuhuma za kujipatia  fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mapema  leo  kupitia mitandao mbali mbali ya  kijamii  baadhi ya  wasamaria  wema  wameeleza kusikitishwa na  kito cha utapeli kinachofanywa na  mhubiri   huyo ambae  amekuwa akiishi katika nyumba moja ya kulala  wageni   ya  Wihanzi mjini  Iringa kuwa amekuwa akiwataka  watu mbali mbali  kutuma  pesa kwa  njia ya  M-PESA kuanzia kiasi cha kati ya  TSh 10,000 na kuendelea iwapo  wanahitaji  kupanga  muda wa kuongea na mhubiri  huyo kupitia  simu ya kiganjani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...