ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, July 5, 2013

MKUTANO MKUU SIMBA SC KUFANYIKA JULAI 20 POLISI



Mkutano Mkuu pia utajadili suala la Kaburu (kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa klabu, Alhaj Ismail Aden Rage na kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Popope.
Na Mahmoud
mkutano mkuu wa mwaka wa klabu ya Simba SC, utafanyika Julai 20, mwaka huu katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oystrebay, Dar es Salaam. Kaimu Makamu Mwenyekiti wa S.S.C., Joseph Itang’are ‘Kinesi’ ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo kwamba, uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika kwa siku mbili mfululizo Dar es Salaam na kufikia tamati jana. Kinesi, anayekaimu nafasi ya Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyejiuzulu miezi mitatu iliyopita, alisema kwamba kwa sasa wapo katika maandalizi ya Mkutano huo wa Kikatiba. Pamoja na kupokea taarifa za msingi za klabu kwa mwaka mzima, Mkutano huo pia utajadili ombi la kujiuzulu kwa Kaburu, ambalo tayari limepata baraka za Kamati ya Utendaji. Lakini Kaburu anaonekana kama kujutia uamuzi wake na katika siku za karibuni amekuwa karibu mno na timu sambamba na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo suala la usajili. Pamoja na kuamua kuhusu Mkutano Mkuu, Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilipitisha suala la kuongezewa Mikataba kwa Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Ofisa Habari wa klabu, Ezekiel Kamwaga. Kikao hicho pia kiliidhinisha kiungo Kiggi Makassy kwenda kutibiwa nchini India kufuatia kuumia katikati ya msimu uliopita akiichezea Simba SC mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma. Taarifa ya Simba SC jana ilisema kwamba kwa sasa klabu hiyo inapanga ahadi na hospitali nchini India kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda huko kutibiwa. Kiggi aliumia akiwa katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka mahasimu, Yanga SC na jithada za kumponya kwa tiba za wataalamu wa nchini zimegonga mwamba na sasa anasogezwa mbele. Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba, Simba SC inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia Agosti 5 hadi 11, mwaka huu kuelekea tamasha la kuazimisha siku ya klabu ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day. Katika wiki hiyo, mabingwa hao wa zamani wa Bara watatembelea kituo cha watoto yatima na kuwafariji kwa misaada, watatembelea wagonjwa, watahudhuria kozi maalum iliyoandaliwa na wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro, watatembelea shule kuhamasisha watoto kupenda soka na hususan klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, watatembelea vyombo vya habari kuimarisha uhusiano na kufanya ibada maalum klabuni kwao, kuwarehemu wachezaji, viongzi, wanachama na wapenzi wa tmu hiyo waliotangulia mbele ya haki na kujiombea mema siku zijazo.  Katika hatua nyingine, Simba SC imesema Chuo Kikuu Huria kimekwishawakabidhi makabrasha ya awali ya Mpango Mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo na Kamati ya Utendaji itakutana Julai 13 kuipitia, kabla ya kuirejesha kwa watalaamu wao hao ili ikamilishwe tayari kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...