Emmily Omari akiwa selo.
MREMBO
mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar
anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni
alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo.
Emmily
ambaye amekuwa akiwatesa askari polisi ambao wamekuwa wakimkamata mara
kwa mara na kumfikisha mahakamani lakini haachi tabia hiyo, alipandishwa
katika Mahakama ya Jiji na kusomewa mashtaka yake.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.
Hakimu huyo baada ya kumuona tena Emmily mbele yake akikabiliwa na shitaka
lilelile, alimuuliza alikuwa na tatizo gani lililosababisha mara kwa
mara afikishwe mahakamani hapo, mrembo huyo hakujibu chochote. “We
Emmily sasa unatuletea utani, kila siku unaletwa hapa tunakupiga faini
unalipa unatoka na kwenda kurudia hiyo biashara yako… sasa tunaona kama
unatufanyia masihara sasa leo hakuna cha faini wala dhamana uende
Segerea ukale dona la bure labda utajifunza,” alisema Hakimu Lyon na
kuwaamuru askari wampandishe kwenye Karandinga kwa ajili ya safari ya
gerezani.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.
No comments:
Post a Comment