ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, July 15, 2013

POLE WJTZ, POLE TANZANIA



 
Tanzania ni nchi ya AMANI.Tanzania ni mfano kwa nchi nyingi za Afrika katika kuendesha mambo yake kitaifa na kimataifa. Tanzania imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kisiasa na kijeshi kwa majirani zake kuhakikisha nao wanakuwa na amani na salama. Ukiuliza Msumbiji watakuambia, ukiuliza Zimbabwe, South Africa, DRC, Lebanon, Madagasca, Siera Leon, Darfur na kwingineko bila kusahau Uganda. Rafiki yangu mmoja wa Rwanda aliwahi kuniambia miaka ya nyuma kuwa katika katika nchi zinazoogopeka Afrika kwa kuwa na jeshi nzuri na siasa imara ni Tanzania.
Tuonapo picha hii tuwakumbuke makamanda wetu waliokuwa wanatuwakilisha huko Darfur na kuuwawa na wale wasioamini usawa kwa kila binadamu. Tuungane na familia na ndugu zetu wanajeshi ambao kwa kujitolea kwao ili sisi tutembee vifua mbele kwa sifa na kuishi kwa uhakika tukijua kwamba tuna ulinzi madhubuti, tuwaombee hawa ambao leo wamelala katika mauti, mauti ambayo yamewakuta wakiwa kazini, wakiwa wanawalinda wale wanaochinjwa bila huruma. Tumwombe Mungu azirehemu roho zao na awatie nguvu familia waliopotelewa na wapendwa wao katika kipindi hiki kigumu.
Tunapojivunia amani yetu, wapo ndugu zetu ambao wameweka roho zao rehani kwa ajili ya usalama wetu. Kwa kufa kwao wakiwa katika harakati za kulinda amani sisi tuongeze uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kuendelea kutunza amani ambayo wengi wanaitamani lakini hawaipati ila kwa mtutu wa binduki.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IDUMISHE AMANI YA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...