TAARIFA ZA KUVAMIWA WAKILI WA MUME WA JOYCE KIRIA, PETER KIBATALA .... UKWELI NI HUU HAPA
Nikiwa na wakili wa Mume Wangu, Peter Kibatala na mwandishi wa habari Makene.
Hivi ndivyo alivyojibu wakili wa mume wangu Henry Kilewo, Wakili msomi Peter Kibatala
Goodmorning:nimepigiwa
simu kadhaa toka kwa watu mbalimbali wakinijulia hali baada ya kusoma
some post huko Jamii Forum kwamba nimevamiwa,kupigwa na kujeruhiwa na
watu wasiojulikana kuhusiana na case ninazoendesha kuwatetea
Wanaharakati kadha wa kadha.
Nawapa pole wote waliostushwa na taarifa hizi.
Ukweli ni kwamba niko salama,nimerudi jana usiku tokea Tabora nilikoambatana na Joyce Kilewo Kiria.
Nitaendelea kufanya kazi zangu kama wakili kwa maadili ya uwakili bila
hofu iwayo yote.Ninasubiri kupangiwa tarehe na Mahakama Kuu kanda ya
Tabora kuhusiana na maombi ya marejeo niliyoyawasilisha baada ya uamuzi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora kuwa haina uwezo kutolea maamuzi
hoja zetu za kisheria juu ya mashtaka yanayowakabili Henry John Kilewo
na wenzake.
Siamini kwamba Tanzania kunaweza kuwa na utaratibu wa kuumiza Mawakili wanaotekeleza majukumu yao ya kisheria.
Post hii naitoa toka Mahakama Kuu Dar es Salaam ninakosubiria
kuhudhuria case nyingine kwa mujibu wa majukumu yangu ya kila siku.
Viva Freedom.
Peter Kibatala,
Advocate.
No comments:
Post a Comment