ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, July 14, 2013

THIAGO ALCANTARA AITOSA RASMI MAN UNITED - AJIUNGA NA BAYERN MUNICH


Hatimaye kiungo wa kimataifa wa Spain na FC Barcelona Thiago Alcantara ameuzwa rasmi kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya na Ujerumani Bayern Munich.

Thiago ambaye alikuwa akihusishwa mno na kujiunga na Manchester United ingawa juzi kocha David Moyes alisema hawakuwahi kusema wanamhitaji mchezaji, amejiunga rasmi ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa 25 million euros.

Mapema wiki iliyopita kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikaririwa akisema kwamba anamhitaji Thiago kwenye timu yake na amewaomba viongozi wake kumsajili mchezaji huyo tu msimu huu.

Thiago amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Bayern Munich.Source: Shaffih Dauda

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...