Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema Tanzania sio mali ya
chama chochote cha siasa wala kundi lolote la watu wakati akihojiwa
katika kipindi cha Makutano na Fina Mango. Mheshimiwa Peter Msigwa
alitoa kauli hiyo alipoulizwa anaonaje mwamko wa kufanya mabadiliko
unaoendelea ikiwemo mchakato wa katiba mpya.
Aliwalaumu watu wa kipato cha kati kwa
kusema wao ndio kikwazo cha maendeleo kwa sababu ya kuridhika na vitu
vidogo walivyovipata, "Kila mtu aingie acheze huu mchezo kwamba ni
wakati uliofika wa kuibadilisha Tanzania, tuibadilishe kifikra. Watu
wengi mmekaa maofisini na kompyuta zenu na vijumba vidogo mmejenga na
vigari vidogo mmeweka nje mnaogopa, lakini kama tutaendelea kuruhusu
akili ndogo iendelee kutawala hatutaenda popote" alisema Mheshimiwa
Msigwa.
Hata hivyo aliipongeza tume ya katiba
kwa kusema ameridhishwa na ilivyofanya kazi yake kutokana na hofu
waliyokuwa nayo baada ya mchakato wa kuandaa katbiba mpya ambao
ulianzishwa na CHADEMA kuchukukuliwa na kugeuzwa agenda ya chama tawala
na hivyo kuleta wasiwasi wa haki isingetendeka hasa ile ya uwakilishi
katika utoaji maoni ya katiba.
Unaweza kumtazama Mheshimiwa Peter Msigwa akiongelea mabadiliko ya
Tanzania kwa kirefu
No comments:
Post a Comment