WANAJESHI WA TANZANIA WALIO UAWA DARFUL WAAGWA
Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony.
Prayers from a chaplain.
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers.
Military salute as the 'Last Post' rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes.
Start of the last journey home.

WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wakati Watanzania wakiendelea
kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa jeshi hilo waliopoteza maisha
katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa kushambuliwa na waasi, nchini DRC
yamezuka mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya Serikali.
Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka
kati ya Wanajeshi wa Serikali na waasi karibu na mji wa Goma, mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia Shirika la Utangazaji
la Uingereza (BBC) kuwa ndege za kivita za Serikali zimefanya
mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku wa kuamkia jana.
Umoja wa mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu,
kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia katika mji wa
Goma.
Raia wakimbia mapigano
Wakati huo huo, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, yamesema kuwa
zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani
ya Uganda, kukwepa mapigano hayo.
Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini Congo, Allied Democratic Forces
walishambulia mji wa Kamango na kusababisha mapigano makali kati yao na
jeshi la serikali.
JWTZ: Askari wetu DRC wapo salama
Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Tanzania (JWTZ), Kanali Mgawe,
alipoulizwa kuhusu mapigano hayo aliwataka wananchi kutokuwa na wasi
wasi kuhusu usalama wa wanajeshi wa Tanzania.
“Wanajeshi wa Tanzania wapo salama hakijatokea kitu chochote tofauti na
kama kuna tatizo lolote tutatoa taarifa, wanajeshi wetu nchini Kongo
DRC wapo salama,” alisema.
Wanajeshi wengine wadaiwa kufa Darfur
WAKATI Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliokufa katika Jimbo la Darfur
nchini Sudani, askari wengine watatu wa jeshi hilo wamedaiwa kupoteza maisha.
Idadi hiyo imedaiwa kuongezeka, baada ya wanajeshi hao watatu ambao ni kati ya 14 waliokuwa wamejeruhiwa vibaya, nao kupoteza maisha katika shambulizi la kushtukiza.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya JWTZ, kimesema kuwa askari hao wamefariki dunia baada ya jitihada za madaktari kuokoa maisha yao kushindikana.
Askari hao walifariki baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi wa
Sudani, walipokuwa katika msafara wa kusindikiza waangalizi wa amani
kutoka Khor Abeche kwenda Nyara, katika Jimbo la Darfur.
MTANZANIA ilipomtafuta msemaji wa jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe
kuzungumzia taarifa hizo, alisema hakuna taarifa zozote zinazoonesha
kuwapo na ongezeko la idadi ya vifo vya Darfur, Sudani.
Kuhusu usafirishwaji wa miili ya askari hao kuja nchini, Kanali Mgawe
alisema suala hilo la usafirishwaji wa miili ya askari hao,
linaratibiwa na Umoja wa Mataifa (UN), ingawa JWTZ inafuatilia kwa
karibu.
“Ninapenda kukuambia kuwa hadi sasa hakuna mwanajeshi aliyeongezeka,
ila hizo ni taarifa ambazo si sahihi na zimekuwa zikienezwa katika
mitandao ya kijamii. Sisi kama jeshi hatuna taarifa kama hizo,” alisema
Kanali Mgawe.
Alipoulizwa kuhusu kutajwa kwa majina ya marehemu waliokufa katika
tukio hilo la kushtukiza, Kanali Mgawe alisema jeshi haliwezi kutaja
majina hayo kwa sasa, ila kinachofanyika ni kuwasiliana na ndugu wa
marehemu hao.
“Safari hii asilimia kubwa ya askari wetu waliokwenda Sudan, wametoka
katika mikoa ya mipakani, kwa hiyo tunachokifanya sasa tumeshawasiliana
na makamanda wa kambi zote za jeshi ambazo wametoka marehemu hawa, ili
waweze kuwasiliana na ndugu wa marehemu.
“Hivi ndugu utajisikiaje unasoma gazeti au unaangalia TV na kusikiliza
redio halafu ukasikia kuwa ndugu yako amefariki utajisikiaje, ni lazima
katika hili tuweze kufuata taratibu nzuri zinazokubalika kwa
kuwasiliana nao moja kwa moja.
“Ninachotaka kuwahakikishia Watanzania kuwa JWTZ lipo imara na kama kuna taarifa yoyote tutaitoa mbele ya umma,” alisema.
Hata hivyo Kanali Mgawe alisema jeshi hilo limetuma ujumbe maalumu
kwenda Darfur kuchunguza kiini cha tukio hilo, ingawa hakuweza kueleza
kikosi hicho kinaundwa na wataalamu wa fani gani.
Source: Mtanzania
No comments:
Post a Comment