Italia bado imendelea kukumbwa na wimbi kubwa la
ubaguzi wa rangi pale Waziri wa Kwanza Mweusi alipotupiwa ndizi alipokuwa
akihutubia katika mkutano wa Chama.
Waziri wa Ushirikiano ni Mwitalia wa
kwanza mweudi aliyeteuliwa hivi karibuni na amekuwa akipata taabu sana kutokana
na dhana ya ubaguzi iliyojengeka miongoni mwa raia wa Italia. Cesile Kyenge ni
mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye amekuwa akipigania haki ya
wahamiaji kupata uraia wa kudumu wa Italia.
Muda mfupi kabla ya tukio hilo siku ya
Ijumaa, wanachama wa mrengo wa kulia Forza Nuova waliandamana wakipinga kampeni ya
Waziri Kyenge ya kutaka kumpa uraia mtu yeyote isipokuwa aliyezaliwa katika
ardhi ya Italia.
“Uhamiaji Unaua” viliandikwa baadhi ya
vipeperushi ambapo ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya Forza Nuova wakimaanisha kuwa
mauaji mengi yaliyofanyika Italia yalisababishwa na Wahamiaji.
Ingawa
ndizi alizokuwa akitupiwa zilimkosa, Waziri Kyenge alijibu katika mtanda wa
kijamii wa twiter “sad” huzuni kwa kutupa chakula hasa katika wakati huu wa
mgogoro wa kiuchumi.“Ujasiri wa kubadilisha hali ya mambo unatoka ndani mwa mtu” alisema waziri Kyenge.
Hata hivyo, Waziri Kyenge amekuwa akikabiliwa na matusi mara kwa mara hata kutoka kwa wanasiasa wengine. Mapema mwezi huu, Mbunge mwanamizi wa kaskazini anayepinga sheria ya uhamiaji alimtukana matusi na kumlinganisha na “orangutan” Hata hivyo aliomba msamaha baadaye
No comments:
Post a Comment