ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, August 16, 2013

MKUTANO WA BARAZA LA KITAASISI LA CHADEMA KWA MAONI YA RASIMU YA KATIBA LILILOONGOZWA NA DR SLAA JIJINI ARUSHA



 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wibrod Slaa akiwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini Arusha
  Wananchi wakifuatilia kwa makini maoni mbalimbali
 Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono kuashiria kukubaliana na maoni ya mwenzao aliyependekeza vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kuondolewa kabisa kwenye katiba mpya na badala yake viongozi wa ngazi hizo wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Zoezi hilo la kutoa maoni lilikuwa linasimamiwa na Dk Slaa
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa akizungumza na wananchi wa Jijini Arusha jioni ya leo katika muendelezo wa Mikutano ya wazi ya Mabaraza ya Kitaasisi ya Chadema kukusanya maoni ya Katiba Mpya kwa upande wa Chadema kama taasisi kamili.

Dr Slaa kwa siku ya leo amefanikiwa kufanya mikutano miine ya wazi Mkoani Arusha na baadae kushiriki katika kikao kingine cha mabaraza hayo cha ndani kilinachoendelea katika hoteli ya New Arusha.
Katika mikutano hiyo Dr Slaa ameambatana na wanasheria wa chama akiwemo Mabere Marando pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu akiwemo mjumbe wa Kamati Kuu Dr Kitila Mkumbo.
Wananchi mbali mbali walipata fursa ya kutoa maoni yao hadharani katika mjumuiko huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, na kujaza eneo la wazi katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa.

 
 Mzee Ole Kisambo, ambaye aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mgaharibi akitoa maoni yake kwa Dk Slaa.
Mzee OleKisambo, ambaye aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mgaharibi akitoa maoni yake kwa Dk Slaa.
 Mwanasheria wa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Wakili Mabere Marando akichambua baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba inayokusudiwa kutolewa maoni na wananchi. Marando amesema kwa upande wa Chadema wanaunga mkono zaidi ya asilimia 80 ya mambo yaliyomo katika rasimu hiyo iliyoandaliwa na Tume inayoongozwa na jaji Warioba.
 Mratibu wa vikao vya mabaraza ya Chadema, mh Mwita Waitara akisalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Wakili Mabere Marando ambye pia alimkaribisha Dk Slaa
 Wanasheria vijana wakiwafafanulia wananchi vipengele mbalimbali vya rasimu ya Katiba. Mwenye suti ni James Lyatuu na mwenye tisheti ya mistari ni Mathias Lyamunda
 Walemavu pia walipata nafasi kuwasilisha maoni yao…
 Mmoja wa kina dada waliojitokeza kutoa maoni yao pia
 Kulikuwa na fomu nyingi zilizogawiwa kwa wananchi wengine kutoa maoni yao kwa kuandika kama huyu
 Jukwaa kuu nao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa kujaza fomu maalum
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusiana na rasimu ya Katiba Mpya
 Viongozi wote na wananchi walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kama ishara ya kumbukumbu za wananchi waliouwawa kwa kulipukiwa na mabomu katika mkutano wa chadema jijini Arusha kwenye uwanja wa Soweto Juni 15, 2013.

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa  akibadilishana taarifa na viongozi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, wakati huo huo Marando akizungumza na Ally Bananga

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...