Mwanamke mmoja wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 34 amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Harare akiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya dola 45,000 akitokea India.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa Msichana huyo alikamatwa na madawa ya kulevya yenye uzito wa kilo 15 aina ya ephedrine. Msichana huyo alifika Harare akitokea India kwa shirika la ndege la Emirate.
Alipowaonyesha passport yao na maafisa wa uwanja wa ndege kuona anatokea India kuelekea Afrika Kusini walijua fika hiyo ni route ya madawa na kweli walipompekuwa walimkuta na bahasha za khaki 30 zenye unga huo
Vijana wetu wengi wamekuwa wakienda bndeni kutafuta maisha, matokeo yake wanaenda kutumiwa kama punda wa kusafirisha mzigo wa madawa ya kulevya. Wengi wamerudisha Tanzania wakiwa marehemu.
Tunafanya nini kuwaelimisha vijana wetu juu ya hili? Taifa linaangamia na nguvu kazi inapotea na sifa yetu inazidi kuporomoka.
No comments:
Post a Comment