ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, August 14, 2013

Nape:Madiwani wa CCM waliofukuzwa Kagera waendelee na kazi

  
Sakata la kufukuzwa kwa madiwani nane wa chama cha mapinduzi(CCM)  Mkoani Kagera limechukua sura mpya baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa anayeshughulikia itikadi na uenezi Nape Nnauye kusema madiwani hao waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida na ni madiwani kisheria kutokana na kikao cha Halmashauri kuu ya Mkoa wa Kagera kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja kuwafukuzisha uwanachama madiwani hao
Bwana Nape amefafanua kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa wabunge na madiwani kuwa uamuzi wa Halmashauri kuu ya Mkoa siyo wa mwisho na uamuzi huo unapaswa kupata baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe,hivyo madiwani hao ni halali mpaka kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti ambacho kitatoa maamuzi kuhusu suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...