Katibu wa jumuia na taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda  anatarajia kuunguruma kesho kwenye uwanja wa ndege maarufu kwa jina la K. ndege mjini Morogoro mara baada ya swala ya Ijumaa saa 8 mchana. Mkutano huo umeandaliwa na umoja wa wahadhiri wa Kiislam Tanzania.

Katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa. Mashekh kibao watakuwepo ikiwemo Sheikh Kondo Bungo. Kwa hamasa iliyopo watu watajaa ile mbaya kama unavyojua sheikh Ponda ni kipenzi cha waislam. Kama kawaida kwenye mikutano ya waislam, amani itatawala. Wote mnakaribishwa.