Sakata la klabu ya Yanga kugomea kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya Ligi na Azam Media wa kuipa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za ligi kuu kituo cha Azam TV limechukua sura mpya baada ya Rais wa shirikisho la soka la nchini TFF Leogdar Tenga kuingilia kati. (HM)
Kwa mujibu wa taarifa rasmi mtandao huu ulizozipata ni kwamba Tenga amewaandikia barua Yanga akiwaambia kwamba amepata malalamiko yao dhidi ya mkataba wa urushwaji wa matangazo ya mechi za ligi kupitia Azam TV.
Pia Tenga amewaambia Yanga kwamba ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo namna mchakato mzima wa ugawaji wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia maamuzi ya kuingia makubaliano na Azam TV.
Tenga amewaomba Yanga kuwa wavumilivu ili kushughulikia malalamiko yao kuhakikisha muafaka unafikiwa kwa ajili ya manufaa ya soka la Tanzania. Chanzo: shaffihdauda
No comments:
Post a Comment