Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania
Katika Bunge la Afrika Mashariki Adam Kimbisa akieleza kwa waandishi wa
Habari sababu iliyopelekea wao kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati wa
vikao vya bunge hilo, wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara
ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni mbunge wa bunge la
Afrika Mashariki Nderakindo Kessy.
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki
Nderakindo Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wakati wa
mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar
es Salaam.
Katibu
wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji
akifafanua jambo kuhusu Msimamo wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo
kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko, wakati wa mkutano na
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah
Mwambene
Baadhi
wa waandishi wa habari wakiwasikiliza wabunge wawakilishi wa Tanzania
katika Bunge la Afrika Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa
Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
--
Bunge
la tatu la Afrika Mashariki lilikuta vikao vya Bunge vikifanyika kwa
njia ya mzunguko kwa nchi 4 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi) pamoja na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya
Jumuiya.
Katika
kikao cha Kamati ya Uongozi, Wabunge wa Tanzania walitoa pendekezo
kwamba vikao vya Bunge kwa mwaka huu wa fedha August 2013 –June 2014
vifanyike Arusha, kwa vile tayari kuna makazi ya kudumu yaani jengo
jipya lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kiwanja
kilitolewa na Serikali ya Tanzania.
Hata
hivyo Wabunge wenzetu walipendelea vikao vya Bunge viendelee kwa
mzunguko na Wabunge Watanzania tuliendelea na msimamo wa vikao kufanyika
Arusha.
Motion
ililetwa Bungeni na mwenzetu kutoka Kenya kuhusu vikao vya Bunge
kufanyika kwa mzunguko….Spika alimwambia mleta Motion kufuata kanuni
ambapo ilitakiwa mjadala wake uendelee katika kipindi cha masaa 24 baada
ya kuwasilisha.
Wabunge
wenzetu hawakukubaliana na uamuzi wa Spika na kuamua kutoka nje na
kusababisha kikao cha Bunge kuahirishwa mpaka siku inayofuata.
Kwa
utaratibu wa kanuni za Bunge, iwapo nchi moja isipokuwa na Wabunge
wasiozidi zaidi ya watu basi kikao cha Bunge kinavunjwa kwa dakika 15 na
Bunge kuanza tena na baada ya hapo ikiwa bado akidi ikiwa haitosh,
kikao cha Bunge huvunjwa mpaka siku inayofuata.
Wabunge
wa Tanzania tuliamua kwa pamoja kuwa na msimamo wa kutoka ndani ya
Bunge kwa kuonyesha kusikitishwa na kitendo cha wenzetu kumdhalilisha
Spika wa Bunge pamoja na kuonyesha msimamo kwamba Wabunge Watanzania
vile vile tuna msimamo na hatukubali kuyumbishwa.
Baada
ya hapo, ndio tuliweza kukaa meza moja na kufikia makubaliano kwamba
Arusha ipate vikao viwili na Tanzania vile vile ipate kikao kimoja.
Makubaliano hayo yalipelekea Motion ya kutaka vikao vifanyike kwa
mzunguko kufanyanyiwa marekebisho ili kuongeza Arusha kupata Vikao
viwili na Tanzania kimoja sambamba na nchi zingine za Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi kupata vikao kwa njia ya mzunguko.
Vikao
vya Arusha vina umuhimu sana kwani ni Kikao cha Bajeti kitasaidia
kupunguza gharama kubwa kwani wafanyakazi wa Secretariet, Maafisa pamoja
na vitabu vya bajeti na vitendea kazi havitasafirishwa nchi yeyote
isipokuwa vitabaki Arusha. Hali kadhalika kikao cha Ukaguzi vile vile
kitapunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Adam Kimbisa
Mwenyekiti
No comments:
Post a Comment