Mwakilishi
wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012,
Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini jana kwenda nchini Indosia katika
kambi ya Miss World 2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii
tayari kwa safari hiyo.
Akiongea
na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa
uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo
huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi
hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International
Agency, Hashim Lundenga akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya
kuondoka.
Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege jana
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege jana
Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia jana.
No comments:
Post a Comment