"Nawashukuru wananchi wamenipa
ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge
wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne,
ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk.
Kingwangallah. Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi
amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo kwa kuwataja
majina vigogo wanaojihusisha na dawa za kulevya na kwamba bado anasubiri
kujibiwa. Dk. Kigwangallah amekabidhiwa majina hayo siku chache tu
baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), William Lukuvi,
kulieleza Bunge kuwa kama serikali itaamua kutaja wanaojihusisha na
biashara hiyo hakuna atakayesalimika ndani ya bunge kwa sababu pia wamo
wabunge wanaotajwa.
ADV
SOMA HABARI
Monday, September 2, 2013
Nimepewa majina ya wabunge wauza dawa za kulevya: Wamo CCM, Chadema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment