Maelfu ya wakazi wa Mwanza na miji ya jirani wakimsikiliza Rais Kikwete katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na
miji ya jirani katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.Rais
Kikwete yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa na kubonyeza kitufe
kuashiria kuzindua mradi wa kufua umeme wa megawati 60 huko
Nyakato,Mwanza leo asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini
Profesa Sospeter Muhongo.Uzinduzi wa mitambo hiyo ni sehemu ya ufumbuzi
wa tatizo la umeme uliokuwa unaikabili kanda ya ziwa.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kufua umeme wa megawati
60 muda mfupi baada ya kuzindua mitambo hiyo huko Nyakato Mwanza leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia akiwa na mavazi maalumu) akikagua
jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani mwanza
leo mchana.Picha na Freddy Maro
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumapili, Septemba 8, 2013, amezindua mtambo wa kufua umeme kiasi
cha megawati 60 katika eneo la Nyakato mjini Mwanza, umeme ambao
utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza shida ya umeme katika Mkoa wa
Mwanza na mikoa ya jirani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua
rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu terehe 7.9.2013.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na
Kanali Mstaafu wa Jeshi, Shadrack Faustino Mbilizi aliyehudhuria sherehe za
ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye huko Magu na pia alipokea kupokea kadi
yake ya kitambulisho cha matibabu kwa wazee.
Rais Jakaya Kikwete akipokea
kitambulisho cha matibabu kwa wazee kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu
Mheshimiwa Jaqueline Liana kwa ajili ya kupewa Kanali Mstaafu Shadrack Mbilizi
na mkewe Mariam Said wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya
Lugeye tarehe 7.9.2013.Picha zote na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment