ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, September 11, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Aongoza Ufunguzi Wa Maonesho ya Bidhaa Zinazozalishwa nchini China Jijini Dar es Salaam


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijaribu jembe la kupandia nafaka wakati alipotembelea banda la kiwanda cha Qingyuan  Manchu Autonomous County cha nchini China wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Wanaomtazama ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto)  na  Balozi wa China nchini LV Youqing (kulia).
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (katikati) akiongea na viongozi kutoka nchini China leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa maonyesho  ya bidhaa zinazozalishwa nchini  humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini  China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo waweze kufanya biashara na watanzania. Kulia kwa waziri mkuu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na kushoto kwake ni Balozi wa China nchini LV Youqing.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia mfano wa nyumba zinazojengwa na kampuni ya Beijing New Building Material alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wapili kulia  ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na watatu kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara 

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia malighafi zinazotumiwa na  kampuni ya  Beijing New Building Material kutengenezea nyumba alipotembelea banda hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza  kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa  wa Kampuni hiyo Alec Lu na wapili kulia ni Makamu Meneja Mkuu Fred Yu.
 Mfanyakazi wa kiwanda cha Changzhou Amec Group cha nchini China Yan Xing Long (kulia) akimueleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda jinsi mashine ya kuchanganya kokoto iliyotengenezwa na  kiwanda hicho  inavyofanya kazi  wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa watu mbalimbali walioshiriki  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne ambayo yamefunguliwa jana yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo yaweze  kufanya biashara na watanzania.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...