BANGKOK (AP) —
Ndege ya abiria ya Thai Airways ikiwa imebeba zaidi ya abiria 280
imepata ajali wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Bangkok na
kujeruhi watu 14
Muda
mfupi baada ya ajali hiyo kutokea wafanyakazi wa ndege hiyo
walilazimika kuondoa nembo (logo) ya ndege hiyo upande wa mkia na
ubavuni ikiwa ni hatua ya kulinda hadhi yake na kutojichafulia jina
Ndege hiyo Airbus
A330-300 ilikuwa ikitokea Guangzhou, China na ilipata hitilafu kwenye
matairi wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege jana usiku, na kwamba
abiria wote waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi
No comments:
Post a Comment