UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam leo uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar
kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya
kutimia kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
timu hizo zikitoka 1-1.


Baada
ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa
Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa
viti na kuvitupia uwanjani.
Mara
moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu
ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa
pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe
kwa kusindikizwa na Polisi.
Katika
mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mohamed Theofile wa Morogoro
aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, ambao
walishindwa kuumudu kabisa, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa
bao 1-0.
Bao
hilo lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe
dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri ya Betram Mombeki na kumpiga
chenga beki Salum Kanoni, kabla ya kumchambua kipa Hannington
Kalyesebula.
Kagera
ilipata pigo mapema dakika ya 22 kipa wake Agathon Anthony kuumia
katika harakati za kuzuia shambulizi la Tambwe na nafasi yake
ikachukuliwa na Mganda, Kalyesebula.
Kwa
ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza, ingawa
Simba SC ndiyo waliotengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.
Kipindi
cha pili, Simba SC iliendelea kusukuma mashambulizi mengi langoni mwa
Kagera, lakini washambuliaji wake walikosa umakini wa kutumia nafasi.
Kagera
nayo iliendelea kushambulia na kwa ujumla mchezo ulizidi kunoga kadiri
muda ulivyokuwa ukisonga mbele kutokana na ushindani mkali.
Wakati
refa wa akiba, Hussein Kalindo wa Kinondoni, amekwishaonyesha dakika
nne za nyongeza, Kagera ikafanya shambulizi langoni mwa Simba na Daudi
Jummane akaangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Simba SC, Joseph
Owino na refa akaamuru penalti.
Beki wa zamani nwa Simba SC, Salum Kanoni akaenda kumchambua vizuri kipa Abuu Hashimu kuisawazishia Kagera dakika ya 90+2.
Baadhi ya mashabiki wa Simba SC.
Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki na kipa wa Kagera Sugar.…
Baadhi ya mashabiki wa Simba SC.
Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki na kipa wa Kagera Sugar
Simba SC;
![]() |
| Wengine wanang'oa viti, wengine wanakimbia kuokoa maisha yao...hivi ndivyo ilivyokuwa Uwanja wa Taifa leo |
Baadhi ya mashabiki wa Simba SC.
Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki na kipa wa Kagera Sugar.…
Baadhi ya mashabiki wa Simba SC.
Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki na kipa wa Kagera Sugar
Simba SC;
Abuu Hashim, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid, Joseph Owino,
Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betram
Mwombeki, Amisi Tambwe na William Lucian.
Kagera
Sugar;
Agathon Anthony/Hannington Kalyesebula dk22, Salum Kanoni,
Martin Muganyizi, Ernest Mwalupani, Malegesi Mwangwa, Zuberi Dabi/Juma
Mpola dk46, Benjamin Asukile/Adam Kingwande dk46, George Kavilla, Themi
Felix, Daudi Jumanne na Paul Ngwai.

No comments:
Post a Comment