BG
Group leo imetanganza kukamilisha kikamilifu majaribio ya uchimbaji
kwenye eneo la gesi la Pweza ndani ya bahari kusini mwa Tanzania, na
kuhitimisha programu kubwa ya kufanya tathmini kwenye Kitalu namba 4.
Hii inathibitisha matarajio ya ubora katika hifadhi hii ya gesi asilia
na kufanya maendeleo chanya.
Hifadhi
ya gesi ya Pwezainakadiriwa kuwa kilometa 70 kutoka kwenye pwani ya
Tanzania kwenye kina cha maji cha meta1 400 . Matokeo ya awali kutoka
kwenye majaribio ya uchimbaji wa gesi kwenye kitalu namba 3 cha Pweza
yamethibitisha kuwepo na hifadhi ya gesi yenye ubora wa hali juu,
Majaribio ya uchimbaji ni utaratibu unaokubalika katika shughuli za
utafutaji wa gesi, na ni utaratibu unaotumika katika kubaini ubora wa
hifadhi ya gesi.
Majaribio
matatu yalifanyika katika hifadhi ya gesi ya Pweza , jaribio la kwanza
lilifanyika kwenye Kitalu namba 4, ambapo mtiririko wa gesi ulikuwa
katika kiwango cha futi za ujazo milioni57 cha gesi kwa siku,
kulingana na uwezo wa mwisho wa kifaa kilichotumika katika majaribio ya
uchimbaji. Muhimu zaidi, majaribio haya yameonyesha kwambavisima
vitakavyochimbwa kwa uzalishaji vinaweza kutiririka gesi kwa kiwango
cha juu na kwamba hifadhi ya gesi ya Pweza kimsingi ina uzalishaji
mkubwa kulinganisha na visima vingine vilivyochimbwa na kampuni ya BG
Tanzania.
Rais
na Meneja Mkuu wa kampuni ya BG Afrika Mashariki, Derek Hudson,alisema:
“Tumefurahishwa na matokeo ya majaribio yetu na tathmini katika Kitalu
namba 4 cha gesi;kuna raslimali za gesi za futi za ujazo wa trilioni4
(tcf). Kazi iliyofanyika inaonyesha gesi yenye ubora wa hali ya juu
kwenye maeneo hayana tunaendelea kushirikiana na washirika wetu
Serikalini na katika sekta binafsi kuhusumatarajio ya kuweka mtambo wa
Gesi Asilia (LNG) , ambapo uzalishaji kutoka kwenye vitalu hivi vya gesi
utakuwa ukitegemea mtambo huu.”
Majaribio
haya katika kisima cha Pweza pia yamethibitisha rasilimali ya
gesiambapo kampuni ya BG hivi karibuni imetangaza kuwa na raslimali za
jumla za gesi nchini Tanzania zinazofikia futi za ujazo trilioni13.
Meli
ya uchimbaji katika kina kirefu iliyokodiwa na kampuni ya BG iitwayo
Deep SeaMetro-1kwa sasa imehamiaupande wa kusini katika Kitalu namba
1ambapo inafanya uchimbaji wa tathmini (appraisal) kwenye eneo jingine
ilipogunduliwa gesi liitwalo Mzia.

No comments:
Post a Comment