Mgomo wa wenye mabasi wasababisha usumbufu kwa abiria.
Mgomo
wa kusafirisha abiria katika kituo cha mabasi ya mikoani na nchi jirani
cha Ubungo jijini Dar-es-Salaam,umezua usumbufu kwa abiria ambao
wamecheleweshwa kwa saa kadhaa kufuatia mgogoro kati ya wamiliki wa
mabasi kupinga utekelezaji wa sheria ya viwango vya uzito unaoruhusiwa
kwenye barabara za hapa nchini .
ITV ilifika kituoni hapo majira ya alfajiri ili
kushuhudia mgomo uliokuwa umeitishwa na chama cha wamiliki wa mabasi ya
kusafirishia abiria Tanzania Taboa, kufuatia serikali kupunguza uzito wa
asilimia tano kwa mabasi na malori kwa asilimia tano yatakayokuwa
yakitumia barabara za hapa nchini, wakiongea na ITV baadhi ya abiria
walikuwa wasafiri na mabasi hayo,wamehoji uhalali wa wao kukatiwa tiketi
za safari na mawakala wa mabasi hayo,ili hali wakijua kuwa,matajiri wao
wamepanga kuendesha mgomo huo hivyo kuwasababishia usumbufu usio wa
lazima.
Naibu katibu mkuu wa TABOA bwana Severine Ngalo
amesema kuwa watasitisha ukatishaji tiketi kwa abiria kama serikli
itashikilia msimamo huo,na kudai kuwa katika nchi za afrika mashariki
hakuna utaratibu wa mabasa ya abiri kupimwa katika mizani barabarani
huku wakisema kuwa uataratibu huo unakwamisha ushindani wa soko katika
nchi za Africa mashariki.
Afisa katika chama cha kutetea abiria Tanzania
bwana Gervas Lutaguzinda amesema kuwa,wamiliki hao wasitumie abiria kama
ngazi ya kufikishia matatizo yao kwa serikali,huku mkurugenzi wa
barabara toka mamlaka ya udhibiti wa uasfiri wa majini na nchi kavu
Sumatra wakidai kuwa watawafutia leseni wamiliki watakao kiuka mkataba
wao na mamlaka hiyo.
amesema hatabadilika kwani anasimamia sheria na
anayetaka kugoma aendelee kugoma lakini asipeleke gari lake
barabarani,hadi ITV inaondoka katika eneo la tukio katika kituo cha
mabasi Ubungo mabasi ya abiria yalikuwa yameanza kuondoka kituoni hapo
majira ya saa tatu asubuhi,kukiwa na makubaliano ya kutokupitia sehemu
za mizani siku ya leo .

No comments:
Post a Comment