
.Mabadiliko hayatakuja kwa kubadilisha vyama bali ni nia zenu {Mindset) zikifanywa kuwa mpya na mapenzi ya nchi yenu.”
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Bi. Mariam Mungula akiwa
pamoja na uongozi wa tawi la CCM UK wakimpa “tour” ya London Underground
train (Tubes) Naibu katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba (MB)
katika ziara yake hapa Uingereza.
Naibu
katibu Mkuu CCM Taifa Mh. Mwigulu Nchemba akitembelea London
Underground Trains (Tube) Kujionea Jinsi nchi za magharibi zilivyopiga
hatua za kimaendeleo huku akiambatana na Uongozi na Marafiki wa CCM tawi
la Uingereza.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Ndugu Maina Owino akimpokea
Naibu Katibu Mkuu wa CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba mara alipowasili kwa
ajili ya mkutano na wanachama wa CCM hapa United Kingdom.
Baadhi
ya Viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la Uingereza
wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa St. Patrick Jijini Leicester
wakisubiri kuwasili kwa Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba.
Ndugu Abraham Sangiwa
wa Itikadi, Siasa na Uenezi Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza
mwenye skafu ya Tanzania na bendera ya CCM wakibadishana mawazo na Ndugu
Mwaupete Upete Mwenye suti Nyeusi wa Uchumi na Fedha CCM tawi la Uingereza nje ya ukumbi wa St. Patrick – Leicester Uingereza kabla ya Mkutano wa wanachama wote wa CCM hapa UK na Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Ndugu Mwigulu Nchemba (MB).
Mtoto
wa Katibu wa CCM shina la Jiji la Leicester Uingereza (Ndugu Moses
Kusamba) akimkaribisha Mwigulu Nchemba Kuwasikiliza wanachama wake kwa
nyimbo za kitaifa na chama.
Mkutano wa wanachama ukiendelea kwa wajumbe kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao.
Watanzania na wana CCM Wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Mh. Nchemba kwa Makini
Mshauri wa Rais Ndugu Rajabu Luhwavi akifafanua Jambo ndani mkutano wa wanachama wa CCM hapa Uingereza.
Katibu
wa CCM shina la Birmingham na Mwenyekiti wa kamati ya Maadili tawi la
Uingereza Bi. Lilian Barongo akiwa pamoja na Mwenyekiti shina la
Northmpton Dr. Abdalah Saleh na Bi. Rose Kiputa Katibu Shina la Cardiff –
Wales.
Mwenyekiti
wa shina la CCM SOUTHMPTON Ndugu Kapinga Kangoma akiteta na BEN TV Nje
ya Ukumbi wa Mkutano Jijini Leicester – Uingereza. (Posted by: Abraham Sangiwa – Deputy Secretary Ideology and Publicity CCM – UNITED KINGDOM).
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Mbunge wa Iramba Magharibi
Mh. Mwigulu Lameck Nchemba akisisitiza Jambo katika hotuba yake
aliyoitoa hapa nchini Uingereza iliyojaa mapenzi na Tanzania zaidi ya
Itikadi na kupokelewa vyema na watanzania wengi hapa UK.
Katika
hali iliyotajwa kuwa ni ya furaha, kutokana na changamoto zilizokuwepo
siku ya jumamosi jijini Leicester Uingereza, kijana shupavu na “JEMBE”
la kujivunia katika Taifa la Tanzania Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, na
Mbunge wa Ilamba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba
akiambatana na mshauri wa Rais mheshimiwa Rajabu Luhwavi, kwa pamoja
waliweza kutoa majibu ya changamoto nyingi zinazolikabili Taifa kwa
watanzania wengi waliojitokeza katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa na
watanzania wengi kutoka maeneo mbali mbali ya Uingereza.
Ujasiri,
uwazi na ukweli wa mambo ya kiutendaji katika taifa letu ndio hasa
imekuwa ni chachu na kivutio kikubwa kwa watanzania wengi waliohudhuria
mkutano huo mkubwa jiji Leicester ambapo Mh. Mwigulu Nchemba aliweza
kuweka wazi mengi ambayo serikali imeweza kuyafanya katika upande wa
Elimu, Miundo mbinu na huduma za afya kwa watanzania pia kutoa kasoro
katika maeneo yanayokuwa vikwazo katika kutoa huduma bora.
“Nchi
yetu ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya, mojawapo ya mambo
ambayo tunayafanyia kazi ni suala la uraia pacha. Ni pendekezo
lililowakirishwa na Chama Cha Mapinduzi katika baraza zake za uchangiaji
maoni ya Katiba mpya. CCM inawajali watanzania wote hivyo ikaona ni
vyema na nyinyi mlioko ughaibuni kupata fursa sawa za kimaendeleo katika
nchi yenu” alisema Mhe. Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa
Nchemba aliendelea na kusema kwamba nchi yetu inapita katika kipindi
cha mabadiliko. Idadi ya watanzania imeongezeka kwa kiasi kikubwa na
wengi wa ongezeko hili ni vijana ambao ni watafutaji na wajasiliamali
wengi. Kuna haja kubwa kama chama kubuni taratibu nzuri za kimaendeleo
ili kuendana na wimbi hili la ongezeko la watu.
Mheshimiwa
Nchemba kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi aliwasihi watanzania waishio
Uingereza kutumia upeo (Exposure) waliyonayo katika kulisaidia taifa
kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kuliko kuwa na ushabiki wa siasa kama
ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa nyumbani na badala yake wawe chemichemi
ya mawazo ya kimaendeleo katika nchi yao.
Watanzania
mlioko nje mna nafasi kubwa ya kuchangia mawazo ya kujenga taifa lenu
la Tanzania, nitawakilisha hoja yenu ya kupatiwa njia ya kuwakilisha
mawazo yenu ama jambo lolote lenye busara na utendaji wa mabadiliko
katika nchi yetu ya Tanzania ili pia mpate fursa ya kuwakilisha maoni na
hoja za haja za kuleta mabadiliko. Kutokuwa na jukwaa lenu la
kuwakilisha hoja zenu za kamandeleo ni kosa. Wazo lolote la kujenga
lazima liwakirishwe katika vikao rasmi kama mchango wa CCM diaspora,
liongeza Mheshimiwa Nchemba.
Tengenezeni
ajenda kulingana na ukomavu na upana wenu wa kimawazo ambao mnaupata
katika nchi hizi za Magharibi ambazo zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo
kutokana na desturi zao za kuthamini, kujituma na kutenda kazi zao kwa
uadilifu mkubwa kwa mapenzi na nchi zao ili kuchangia utekelezaji wa
sera ya chama katika nchi yetu kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu,
miundombinu , sheria n.k. na mimi naahidi tutatengeneza na kuboresha
uwanja mzuri wa mawasiliano kati yetu aliongeza Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba.
Mheshimiwa
Nchemba pia alisisitiza upendo na umoja baina ya watanzania na kuwaomba
wawe kitu kimoja na akawataka wana CCM Uingereza kuwa chachu ya
kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa na vyama
vyao. Mheshimiwa Nchemba pia amekuwa akikonga nyoyo za watanzania wengi
kulingana na utashi na ufahamu wa kujibu maswali kiufasaha, wazi na kwa
uhakika pale alipoulizwa katika mikutano yake iliyofanyika katika
majiji ya Leicester, Northampton na London nchini Uingereza.
Katika
mkutano uliofanyika jijini Leicester watanzania wengi waliuliza maswali
yanayohusu Katiba , Utawala wa Sheria wenye haki sawa kwa wote kama
ilivyo katika nchi za kimagharibi, Uraia pacha, Kurugenzi
inayoshughulikia masuala ya Diasprora ambayo badala ya kuwa kiunganishi
imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wanadiaspora kutokana huduma mbovu zenye
kutokujali na majivuno kutoka kwa watendaji wake wakuu, Tunashauri
watendaji katika kitengo hiki watokane na wanadiaspora wenyewe kwani
upeo (exposure) wao kiutendaji utaleta ufanisi kuliko ilivyo sasa hivyo
kuleta mchango wao kwa maendeleo ya Taifa. Pia Watanzania hao na wana
CCM wameishauri serikali kubadirisha taratibu zake za kiajira katika
Balozi zetu za nje kwa kuwatumia watanzani wenyeji wa maeneo hayo ili
kupunguza mzigo wa gharama serikali, kuongeza ufanisi kwani uelewa wa
kufanya kazi katika mazingira wanayoishi wanaufahamu vyema zaidi kuliko
kuleta watendaji wote katika Balozi zetu kutoka nyumbani.
Vilevile
katika mkutano uliofanyika jijini Northampton siku ya Jumapili, mengi
ya maswali yaliyoulizwa na watanzania waishio katika jiji hilo ni kama
katika masuala ya usalama wa nchi na raia wake dhidi ya matukio ya
tindikali na majanga ya mabomu kule Arusha, tukio la kigaidi hivi
karibuni nchini Kenya na utayari wa nchi yetu katika kukabiliana na
wimbi kama hilo endapo litatokea nchini kwetu, mikakati ya kupambana na
madawa ya kulevya pamoja na lile gonjwa sugu la rushwa.
Akijibu
kwa ufasaha maswali hayo Mheshimiwa Rajab Luhwavi ambaye anaambatana na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, katika ziara
hii, alianza kwa kuwahakikishia usalama wa taifa Watanzania waliofika
katika mkutano huo na kuwaondoa hofu hiyo. Na kuwajulisha kwamba
serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na uhalifu wa aina hiyo
na kwamba taratibu za lazima zinafanyika na hali ni shwari.
No comments:
Post a Comment