Mwandishi wa habari wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, katika moja ya matukio ya kikazi hapa nchini.
Alfajiri ya jana, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.
Akizungumzia suala hilo, kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya jana.
Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro (mama mkwe) ili awasuluhishe
Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanawe na ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....
Alipomuua mama huyo, mwanaume huyo alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Muuguzi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni
cha ITV, Ufo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi
kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake Kibamba
jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia
alimuua mama yake na kisha kujiua.
Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.


Wafanyakazi hao wakibadilishana mawazo hapa na pale katika hospitali ya Muhimbili leo hii

No comments:
Post a Comment