Sehemu ya dawa zilizokama twa katka Operesheni.
Mkurugenzi MKuu wa TFDA na DCI Manumba wakitazama sehemu ya dawa zilizokama
Wadau wa habari wakifuatil
Mkurugenzi MKuu wa TFDA na DCI Manumba wakitazama sehemu ya dawa zilizokama twa.
Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA ) imekamata dawa bandia zenye thamani ya TSh.
49,634,733/= katika operesheni maalum ijulikanayo kama Operesheni
GIBOIA iliyoshirikisha Jeshi la Polisi nchini, Shirikisho la Polisi la
Kimataifa (Interpol), Baraza la Famasi, TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD),
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Viwango (TBS), Tume
ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya
Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Rais na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
Operesheni GIBOIA ilifanyika kuanzia tarehe 1-3
Oktoba, 2013 katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni
Mwanza, Shinyanga,
Mara, Geita, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma na Dar es Salaam. Operesheni
hii pia imefanyika sanjari katika nchi saba zilizopo Kusini mwa Jangwa
la Sahara ambazo ni Afrika ya Kusini, Angola, Malawi, Msumbiji,
Swaziland, Zambia na Tanzania kwa lengo la kupambana na dawa Bandia
Barani Afrika.
No comments:
Post a Comment