ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, October 4, 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA,HUYU NDIYE MHUBIRI WA KIISLAMU ALIYEUAWA KENYA


 
Mrithi wa Al marhum shekh Aboud Rogo aitwae Ibrahim Rogo ameuawa kinyama na watu wasio fahamika nchini Kenya mtindo huu wa uuwaji unafanana na vile Aboud Rogo jinsi alivyouuawa na watu wasiofahamika.Shekh Ibrahim Rogo ameuawa usiku wa kuamkia leo leo akiwa anatokea mskitini,akiwa pamoja na wenzake kwenye gari ndogo,jumla ya watu wanne inasemekana kuuawa kwa kupigwa risasi na watu hao wasiofahamka.Mauaji hayo ya kinyama yametokea wiki mbili tu baada ya tukio la uvamizi wa Wastegate mall mjini Nairobi

Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo 
 
 

WACHOMA KANISA BAADA YA MHUBIRI WA KIISLAMU KUUAWA

 

Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo
Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana wameteketeza kanisa katikaghasia ambzo zimezuka kufutioa kuuwa kwa muhuburi wa kiisilamu. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa keenye ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.

Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.
Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa
Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.
Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.
 
Source:  dj-sek.blogspot
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...