ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, October 28, 2013

VIONGOZI WA EAC KUKUTANA KIGALI RWANDA



ss_96bc6.gif
Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda baadaye leo wanatarajia kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru kinachotarajiwa kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa Kenya -- Uganda hadi Rwanda.
Kuundwa kwa Kituo hicho pia kunatazamiwa kurahisisha shughuli nzima za uchukuzi katika maeneo hayo ya Afrika Mashariki.
Taifa la Sudan Kusini pia linataraji kuidhinishwa kama mshirika katika kikao cha wakuu wa mataifa hayo.
Mkutano huu unalenga kuimarisha maendeleo ya kikanda kupitia kwa miundo msingi bora , uchumi na biashara.

Shughuli hii inakuja baada ya mkutano uliofanyika mjini Kampala Uganda, mnamo mwezi Juni na mwengine uliofanyika mjini Mombasa mnamo mwezi Agosti ambako viongozi walipendekeza kupanuliwa kwa bandari ya Mombasa ili kuwezesha uharaka wa bidhaa kupitishiwa bandarini humo katika kuhudumia kanda nzima

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...