KIUNGO
nyota raia wa Ivory Coast, Yaya Toure amekumbana na kejeli za kibaguzi
akifananishwa na nyani jana usiku wakati Manchester City ikiibuka na
ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya CSKA Moscow katika Jiji Kuu la Urusi.
Kelele
za kibaguzi zilisikika kutoka mashabiki wa wenyeji katika mchezo ambao
City ilinufaika na mabao mawili ya Sergio Aguero ikitoka nyuma na
kushinda mechi hiyo ya Li ya Mabingwa Ulaya.
Na City imethibitisha itapeleka malalamiko rasmi UEFA juu ya ‘unyama’ aliofanyiwa Toure.
“Hakika
inaumiza mtu unapozungumza na watu wanaendelea kufanya
hivyo,”alilalamika Toure. “Huwezi kuamini na inaniumiza sana upande
wangu,”.
Unawasikia wale? Yaya Toure akimuambia refa Ovidiu Hategan juu ya mashabiki waliokuwa wakimuita nyani

Inauma: Toure akiwastaajabu mashabiki wabaguzi

Toure ameitaka UEFA kuchukua hatua kali

Mlengwa: Yaya Toure alikumbana na kejeli za kibaguzi kutoka mashabiki mjini Moscow

Heshima: Toure alivaa beji ya kupiga ubaguzi
“Nafikiri UEFA wanahitaji kufanya kitu cha nguvu. Itakuwa vizuri ikiwa watazuia hiyo.
“Baadhi
ya nyimbo zilizokuwa zinaimbwa zilikuwa za kipumabvu kabisa, nafikiri
UEFA wanatakiwa kufanya kazi. Kila wakati tunasema kitu fulani na
inaendelea, kitu fulani lazima kifanyika kuzuia hii,”.
Alipoulizwa
ni hatua gani ichukuliwe na bodi hiyo ya soka Ulaya, Toure alitaka
adhabu zitolewe badala ya faini ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikitolewa
siku za nyuma.
“Wanahitaji
kufanya zaidi,”alisema. “Nafikiri UEFA wanatakiwa kuwa na nguvu, na
kuzishika klabu zote na mashabiki wote wanaofanya hivyo (wahusika).
Labda kufungia viwanja,”.
“Kwangu kama mchezaji wa Afrikan wakati wote imezungumzwa kusikia kwamba mambo kama hayo tunahitaji kufanya kitu juu ya hilo,”.
Chanzo: Full shangwe
No comments:
Post a Comment