
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.Katika ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Maria Imakulata, Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru Mungu kwa kila jambo.“Tunamshukuru Mungu kwa majaliwa aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba azidi kuijalia umoja katika yote tunayofanya na tunayokusudia kuyafanya,” alisema Mkapa. Mkapa pia aliwashukuru waumini wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua siri kwamba, Kadinali Pengo alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph wakati alipokuwa rais, lakini hakukubali.
Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
“Alichofanya
Rais Mstaafu Mkapa ni cha kuigwa. Tunatakiwa kutambua kuwa hatuishi kwa
nguvu zetu bali kwa uwezo wa Mungu hivyo ni lazima tumshukuru kama
alivyofanya mwenzetu,” alisema Kardinali Pengo.
Baadhi
ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Mawaziri Wakuu
Wastaafu, Edward Lowassa na Cleopa Msuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi na Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine
ni waziri wa zamani, Profesa Philemon Sarungi, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa pamoja wakuu wa
zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Majenerali, Robert
Mboma na George Waitara.
No comments:
Post a Comment