NAPE NNAUYE: KUHOJIWA KWA MAWAZIRI KAMATI KUU YA CCM HAKUKWEPEKI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa
Vwawa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika mji huo
ambao ndiyo makao makuu ya wilaya ya Mbozi, mkutano huo umehudhuriwa na
wananchi mbalimbali wa mji wa vwawa, Katika ziara hiyo Kinana
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye na
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiani wa Kimataifa,
Akizungumza katika mkutano huo Nape Nnauye amesema Injinia Christopher
Chiza Waziri wa Chakula na Ushirika aache kuzungumza na vyombo vya
habari badala yake aandae majibu kwa ajili ya kuhojiwa kwenye kikao cha
Kamati Kuu kwa sababu kuitwa kwake kwenye kamati kuu ya CCM hakukwepeki,
Kutokana na matatizo na malalamiko ya wakulima kuhusu pembejeo,
kukopwa mazao yao na suala zima la wakulima kuikataa mbolea ya Minjingu
huku wakilazimishwa kuitumia.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana,Dr. Asha Rozi Migiro Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa
jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Siasa Itikadi na Uenezi wakipanda miti katika eneo ambalo zahanati ya
kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa inajengwa kwa ajili ya kutunza
mazingira na kuzuia upepo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBOZI
-MBEYA
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Vwawa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa na wanachama wa CCM kijiji cha Ntunduru Kata ya Isansa
Dr. Asha Rose Migiro akiwahutubia wanambozi leo
Wapiganaji Ahmed Michuzi , Richard Mwaikenda na Bashir Nkoromo wakiwa wamepumzika kidogo
Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha Ntunduru
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha Ntunduru
Dr. Asha Rose Migiro akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha Ntunduru
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ntunduru kata ya Isansa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma za asili ya wanyiha
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia kijana Huruma Wiliam
wa Kata ya Isansa wakati alipokuwa akipita kwenye kamba.
Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment