ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, November 5, 2013

Nchemba awaasa Vijana kutafakari uchochezi wa wapinzani


DSC04097
Naibu katibu CCM taifa Tanzania bara na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Shelui Iramba magharibi.Pamoja na kutoa taarifa ya maendeleo yaliyokwishafanyika, Mwigullu alitumia nafasi hiyo kuhimiza maandalizi ya Kilimo kabla ya mvua kuanza kunyesha.
DSC04133
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi,Mwigullu Lameck Nchemba (kulia) akimkabidhi mwenyekiti wa kijiji cha Shelui Saidi Ntunu, moja ya Dawati kati ya 40 aliotoa msaada kwa shule za msingi Shelui na Ntwike.
DSC04092 DSC04093
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shelui wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Mwigullu Lameck Nchemba (hayupo kwenye picha) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara. (Picha na Nathaniel Limu). 
. ili kulinda Amani na utulivu wanchi
Na Nathaniel Limu, Shelui
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigullu Lameck Nchemba amewaasa vijana wa jimboni humo kujenga utamaduni wa kutafakari kwa  undani mambo yanayoenezwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ili kuondoa uwezekano wa kushabikia mambo ambayo yanachangia kuhatarisha amani na utulivu uliopo hivi sasa.
 Mwigullu ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Shelui na kuhudhuriwa na umati mkubwa.
 Amesema CCM kiliridhia kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa nchini lakini mambo na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya siasa na hasa CHADEMA ni kinyume na matarajio ya CCM na Watanzania kwa ujumla.
 Akifafanua Mwigullu ambaye pia ni Naibu Katibu CCM taifa, amesema mambo yanayofanywa au kuenezwa na CHADEMA mengi yanachangia kupandikiza chuki na mifarakano ambayo imepelekea kuvuruga amani na utulivu.
 “Mifano ipo mingi sana inayoonyesha kwamba CHADEMA haipendezwi au imechoka kuwepo kwa amani na utulivu nchini.Hivi karibuni pale Arusha mjini kwenye mkutano wa CHADEMA taifa, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ametwagwa ngumi mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe Huo ndio utamaduni wa CHADEMA”,amesema Mwigullu.
 Amesema kwa hali hiyo vijana au wakazi wa jimbo la Iramba magharibi endapo watashabikia siasa za CHADEMA zenye lengo la kuhatarisha amani na utulivu hapatakuwepo tena na muendelezo wa maendeleo na badala yake ugomvi na migogoro itatawala.
 Katika hatua nyingine Mwigullu amewataka wakazi wa jimbo hilo kufanya maandalizi ya kilimo mapema kabla ya msimu wa mvua haujaanza.
 Mbunge huyo amesema maandalizi hayo yaende sambamba na kufuata maelekezo ya wataalam wa kilimo ili kilimo kiwe na tija zaidi.
 “Sisi wakazi wa jimbo la Iramba magharibi,tujiwekee malengo ya kujitosheleza kwa chakula kwa mwaka mzima Kujitosheleza huko ni lazima tuwe na maandalizi mapema na tujiwekee malengo katika kilimo chetu”,alifafanua.
 Wakati huo huo Mwigullu alitoa msaada wa madawati 40 kwa shule za msingi za Shelui na Ntwike yenye thamani ya zaidi ya shilingi 3.2 milioni.  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...