KIUNGO
wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima raia wa Rwanda,
ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa gazeti la Mwanaspoti, akiwashinda
Amri Kiemba, Shomary Kapombe wa Simba SC na Themi Felix wa Kagera Sugar.
Katika
hafla iliyofana kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wachezaji wengi, mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa
(TEKNOHAMA) Januari Makamba, mchezaji Niyonzima aliondoka na tuzo tatu,
nyingine ya mchezaji wa kigeni na 11 Bora wa Mwanaspti.
Haruna akipokea tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Kigeni kutoka kwa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) |
Katika
tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, Niyonzima aliwashinda mchezaji
mwenzake wa Yanga, mshambuliaji wa Kiganda, Hamisi Friday Kiiza na
mshambuliaji wa Azam kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
Mchezaji
wa Azam FC, Joseph Kimwaga aliwashinda Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na
Ramadhani Singano ‘Messi’ katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji
Chipukizi.
Mwanahamisi
Omar wa Mburahati Queens aliwashinda Shelida Boniface na Fatuma Mussa
katika ya Mchezaji Bora wa kike, wakati Mbwana Samatta aliwashinda Henry
Joseph aliyekuwa anacheza Kongsvinger ya Norway kabla ya kurejea Simba
SC msimu huu na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Thomas
Ulimwengu katika tuzo ya mwanasoka anayecheza nje.
 |
Haruna
akipokea hundi ya Sh. Milioni 5 kutoka kwa Naibu Waziri wa TEKNOHAMA,
Januari Makamba. Wengine kulia ni Zuhura Muro, Mwenyekiti wa Bodi wa MCL
na Tido Mhando kushoto, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCL |
Oden
Mbaga aliwashinda Martin Sanya na Ibrahim Kidiwa katika tuzo ya Refa
bora, wakati Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ aliwashinda
Muingereza Stewart Hall wa Azam na Mholanzi Ernie Brandts wa Yanga
katika tuzo ya kocha bora.
Thomas
Ulimwengu alishinda tuzo ya bao bora alilofunga katika mechi dhidi ya
Ivory Coast kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, wakati Kipre Tchetche
ameshinda tuzo ya Mfungaji bora.
Juma
Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika,
Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Haruna Niyonzima, Themi Felix, Mbwana
Samatta na Kipre Tchetche wameteuliwa katika ’11 Bora’ wa Mwanaspoti.
Zilizotolewa
pia tuzo za heshima kwa wachezaji wa zamani nchini akina Nicholas
Akwitende, John Lyimo, Mbwana Abushiri, Omar Zimbwe, Jellah Mtagwa na
mtangazaji wa zamani maarufu, Mshindo Mkeyenge.
Mkeyenge
aliyeanza kutangza tangu miaka ya 1960 Radio Tanzania (RTD)
aliwahuzunisha wengi baada ya kuwasili jukwaani akiwa amebebwa kutokana
na kukatwa mguu kwa sababu ya maradhi ya kupooza.
Hadhara
Charles alipewa tuzo ya kipaji maalum, wakati Rais wa Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga alipewa tuzo
ya Utawala Bora katika soka. Washindi walipewa na zawadi za fedha,
Niyonzima Sh. Milioni 5, wengine Sh. Milioni 1 na wengine 500,000.
Kwa ujumla tuzo hizo zilizosindikizwa na burudani ya wanamuziki Juma Nature, Joh Makini na King Kiki zilifana.
HAFLA YA TUZO ZA WANASOKA BORA TANZANIA WA GAZETI LA MWANASPOTI ILIVYOFANA JANA MLIMANI CITY
Home
»
Unlabelled
» HAFLA YA TUZO ZA WANASOKA BORA TANZANIA WA GAZETI LA MWANASPOTI ILIVYOFANA JANA MLIMANI CITY
Rais
wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar
Tenga kushoto akimkabidhi tuzo ya Ufungaji Bora mshambuliaji wa Azam
FC, Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast katika tuzo za gazeti la
Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. |
Naibu
Waziri wa TEKNOHAMA, Januari Makamba kushoto akimkabidhi tuzo ya
Mwanasoka Bora, kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima kulia.
Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro |
Rais
wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Said El Maamry
akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje, mwakilishi
wa mshindi wa tuzo hiyo, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC. |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akimkadhi tuzo Refa Bora, Oden Mbaga |
Mshambuliaji
wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella akimkabidhi tuzo ya bao
bora, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe
ya DRC |
Kipa mpya wa Yanga SC, akipokea Tuzo ya 11 Bora kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro kushoto |
Amri Kiemba wa Simba SC akipokea tuzo ya 11 Bora |
Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga akipokea tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi kutoka kwa Mohammed Rweyemamu, Mjumbe wa Bodi ya MCL |
Mwanahaisi
Omar akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike kutoka kwa Makamu Rais wa
Shirikisho la Soka la Wanawake (TWFA), Rose Kisiwa kushoto |
Makamba akimkabidhi tuzo ya heshima, Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Nicholaus Akwitende kulia |
Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, John Lyimo akipokea tuzo ya heshima kulia |
Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Mbwana Abushiri akipokea tuzo yake |
Nahodha mwingine wa zamani Taifa Stars, Omar Zimbwe akipokea tuzo yake ya heshima |
Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Said George aimpokelea tuzo Jellah Mtagwa |
Mtangazaji
maarufu wa mpira wa zamani wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), sasa
TBC, Mzee Mshindo Mkeyenge (katikati) akipokea tuzo yake ya heshima |
Meneja Uhusiano wa Vodacom, Salum Mwalimu akimkabidhi Tenga tuzo ya Utawala Bora |
Wachezaji
na wawakilishi wa wachezaji walioteuliwa katika 11 Bora ya gazeti la
Mwanaspoti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda tuzo zao |
Mzee King Kiki alitumbuiza |
Rapa Joh Makini akitumbuiaza |
Rapa Joh Makini akiwataka waalikwa wainue mikono juu |
Na kweli watu wazima waliiua mikono kucheza Hip hop |
Rapa Juma Nature akitumbuiza |
Ofisa wa Azam FC, Patrick Kahemele akipokea tuzo ya 11 Bora kwa niaba ya Kipre Tchetche |
Juma Kaseja na Amri Kiemba baada ya kupokea tuzo zao |
Msanii akionyesha utundu na kipaji cha kunyumbulika |
Amerudi Yanga huyu; Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado kushoto akifurahia jambo na kipa mpya wa Yanga SC, Juma Kaseja |
Kutoka kulia kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, kiungo wa Coastal Union, Uhuru Suleiman ma mwigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' |
Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayay kulia akiwa na Kaburu |
Ni
haki yake kuchoka; Boniface Wambura kulia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF
anafanya kazi sana na haikuwa ajabu aliishia kusinzia kwa uchovu jana
wakati wa shetehe za tuzo, kushoto ni Mogella.
CHANZO NA BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment