ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, November 2, 2013

Promosheni ya Vodacom Mlimani City "Danganya Toto"

bbb_fdb8e.jpgccc_572e9.jpg
Maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kujipatia simu za promosheni ya Vodacom


Kampuni ya Vodacom leo imeendesha kile ilichokiita ni mnada au promosheni ya kuuza zimu na bidhaa mbali mbali za kielektronic kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 90.
Matangazo yaliyokuwa yanatolewa na vituo mbalimbali hasA Clouds FM yalihamasisha watu na kweli kumekuwa na mwitikio mkubwa sana na watu waliokuwa na shauku ya kujinunulia simu zenye ubora wa hali ya juu kama vile  Apple Ipad 2-64GB, Apple Ipad 2-32GB, Apple Ipad 2-16GB, Samsung Tablet 10.1, ZTE V9 Tablet, BB Playbook 64GB, BB Playbook 32GB, ZTE MF68-Mobile TV, Blackberry 9320, Blacberry 9630, Blackberry 9105, Samsung P520-GSM, Samsung i9003 Galaxy, Samsung i780-GSM, Nokia N97, Sony Ericson Experia, Huawei Phone-V720, Samsung N 150, Desktop Phone G201, K3805 HSDPA Data Car, K3565 HSDPA Data Car, K3570 HSDPA Data Car, Antenna for Router B, Sandisk SD 1GB, PHONE BATTERY 225, Charger V125 & V225, ZTE-Web Box, Router:E5331-Pocke.
Lakini hali haikuwa kama wengi wetu tulivyotarajia. Bei za Simu ni zilezile, au vingineveyo ni uhuni uhuni tu. Nilipoingia kwenye banda la Samsung Tablet nilikutana na mwanadada anayeongea kwa maringo kabisa eti bei zetu sio za promosheni ni bei za dukani. Nikamuuliza, "Sasa wewe umekuja kufanya nini hapa wakati unajua fika watu wamekuja kwa ajili ya promosheni?"  Nilijaribu kuuliza uliza na wengi ya watu walionyesha kushangazwa na bei kubwa tofauti na matangazo halafu pia ufinyu wa bidhaa zenyewe. Mimi binafsi nikisikia promosheni ya Vodacom sintoenda tena kwa kuwa promosheni yao haikuwa "AUTHENTIC"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...