
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa
wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa COP19/CMP9 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa wa Michezo wa Poland, mjini Warsaw. Rais Kikwete alikuwa
anazungumza kwa niaba ya viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika nafasi
yake akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko
ya Tabia Nchi (CAHOSCC).
Rais
Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tokea Januari, mwaka huu,
2013, wakati alipochaguliwa na viongozi wenzake kushika nafasi hiyo
kufuatia kifo cha aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa
Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, Septemba, mwaka jana.
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment