Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante OleGabriel akihutubia Vijana (hawapo pichani) katika
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kujitolea iliyofanyika jijini Dar es
Salaam leo (jana)
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mandisa Mashologu kushoto
akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante OleGabriel mara baada ya kuhutubia katika
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea iliyofanyika jijini Dar es
Salaam leo (jana)


Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante OleGabriel akikagua moja ya baadhi ya mabanda kuangalia
shughuli za kujitolea zinazofanywa na Vijana
NaGenofeva Matemu (Maelezo)
Vijana
watakiwa kuwa na moyo wa kujitolea katika shughuli mbalimbali za
kimaendeleo kwani swala la kujitolea hutoka ndani ya mtu hivyo
kuliepushia taifa kuwa na mzigo mkubwa wa vijana wasiojiweza na kupoteza
nguvu kazi ya taifa.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akifungua rasmi Maadhimisho
ya Siku ya Kujitolea Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha
Utalii leo jijini Dar es Salaam.
Prof.
Gabriel amesema kuwa kuna faida nyingi ambazo zinapatikana kutokana na
ushiriki wa vijana pamoja na watu wengine katika shughuli za kujitolea
ikiwemo ile ya kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la pato la
taifa kupitia shughuli wanazofanya za kujitolea katika jamii.
Aidha akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni “Young Global Active”
ikiwa na maana ya kuwahamasisha vijana kuwa chachu ya maendeleo duniani
kote, Prof Gabriel amewataka vijana wa Tanzania kuhakikisha chachu hii
inaanzia katika taifa lao kwa kujituma na kutumia fursa mbalimbali
zinazojitokeza kushiriki katika shughuli za kujitolea.
Naye
Mkurugenzi msaidizi Kitengo cha Uratibu na Uwezeshaji kwa Vijana
Kiuchumi Dr. Kisui Steven Kisui amewataka vijana kujitambua kwa
kushiriki katika shughuli za kujitolea zinazoendeshwa kidunia ili waweze
kukabiliana na mabadiliko yanayojitokeza katika maisha yao ikiwa ni
njia ya kujikwamua kimaendeleo.
“Kujitolea
kunajulikana duniani kote, kunalipa na kumfanya mtu kupata fursa ya
kujua vitu vingi kutokana na kupata uzoefu na mawazo katika mitandao
mbalimbali ya kujitolea hivyo hatuna budi vijana kushiriki kikamilifu
katika shughuli za kujitolea ili tuweze kuepukana na tamaa zisizokua na
tija katika maisha yetu” amesema Dr. Kisui.
Kwa
upande wake Meneja Miradi kutoka Million Hours Buguruni Youth Center
Bi. Victoria Kululetela kama mmoja wa kijana aliyewahi kujitolea amesema
kuwa kwa kujitolea kwake kupitia kampuni tofautitofauti kulimwezesha
kupata uwezo wa kusimama mbele za watu na kuzungumza, kuweza kuwa
kiongozi mzuri, kuwashawishi vijana wengi zaidi kujitolea katika
shughuli za kijamii na kuwashauri wanawake kuanzisha ujasiliamali
uliowawezesha kuinua kipato chao.
Bi.
Kululetela amewahamasisha vijana kushiriki katika kazi za kujitolea na
kuacha kuangalia zaidi pesa kwani vijana ndilo taifa la leo na ndio
viongozi wa badae hivyo wazingatie kujitolea ili waweze kujulikana na
kuweza kupata fursa nyinginezo zinazopatikana kwa kujitolea.
Kujitolea
kuligundulika kama sehemu muhimu ya maendeleo miaka kumi iliyopita,
mwaka 2001 pale wanachama 126 walipopitisha azimio mwishoni mwa mwaka wa
kimataifa wa wajitoleaji (IVY). Mwaka huu maadhimisho ya siku ya
kujitolea duniani yamefanyika kuanzia tarehe 25 novemba mpaka tarehe 05
desemba yakiwa na lengo la kuwainua vijana kuwa chachu ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment