ARSENAL WAINGIA MKATABA MPYA NA PUMA
KLABU ya Arsenal imetangaza kuingia
Mkataba wa muda mrefu wa udhamini wa vifaa vya michezo na kampuni ya
Puma kuanzia Julai mwaka 2014. (HM)
Pamoja na hayo hakuna kiwango cha
fedha cha udhamini huo kilichothibitishwa Jumatatu, ingawa dili hilo
linatajwa kama kubwa zaidi katika historia ya uhusiani wa Puma na
Arsenal.
Inafahima Washika Bunduki hao
wanapokea kiasi cha Pauni Milioni 30 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini
wakuu, shirika la ndege la Emirates, na imeripotiwa dili hilo jipya
litakuwa sawa na lile ambalo Puma walitoa wakati wanaiponya timu hiyo
Nike, waliokuwa wadhamini wa Arsenal tangu 1994. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment