SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF) limeikumbusha klabu ya Yanga SC kutomtumia kiungo
Athumani Iddi ‘Chuji’ katika mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Komorozine
ya Comoro, wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kuwa bado anatumikia adhabu
ya kadi nyekundu aliyopata kwenye msimu uliopita.
Ofisa
Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto amewaambia Waandishi wa Habari leo
makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba, CAF iliwaandikia
barua kuwakumbusha kuwa Chuji alipewa kadi nyekundu mara ya mwisho
klabu hiyo ilipocheza michuano ya Afrika katika mechi dhidi ya Zamalek
hivyo Yanga haitamtumia Chuji hadi atakapomaliza adhabu yake
Pia
Kizuguto pia amesema hawatamtumia mshambuliaji Emmanuel Okwi japokuwa
CAF imempa leseni ya kucheza michuano hiyo mwaka huu, hadi hapo
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litakapotoa baraka zake.
Okwi
amesajiliwa msimu huu Yanga SC kutoka SC Villa ya Uganda baada ya kugoma
kuendelea kuichezea Etoile du Sahel ya Tunisia iliyomsajili kwa Mkataba
wa miaka kutoka Simba SC ya Tanzania pia.
Okwi alifungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
akilalamika kutolipwa mishahara na Etoile ndipo akaruhusiwa kujiunga na
SC Villa.
Baada
ya Villa kumuuza Yanga ikidai ina haki zote, TFF imeandika barua FIFA
kutaka ufafanuzi kama inaweza kumuidhinisha kucheza Yanga na imeizuia
klabu hiyo kumtumia hadi majibu yapatikane.
Yanga ilitolewa Raundi ya Kwanza katika Ligi ya Mabingwa mwaka 2012
na Zamalek ya Misri, mechi ya kwanza wakilazimishwa sare ya 1-1 Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam Februari 18, na marudiano Machi 3, wakifungwa 1-
0 Cairo.
No comments:
Post a Comment