
Kweli Urais hauna
ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali
popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa ambako Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma
huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge
Maalum la Katiba, leo Ijumaa, Machi 21, 2014.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge
Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya
Kanuni za Bunge Maalum. PICHA NA IKULU.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
jana, Alhamisi, Machi 20, 2014, amewasili mjini Dodoma kwa ziara ya
kikazi ya siku tatu ambako miongoni mwa mambo mengine atakuwa Mgeni
Rasmi na atahutubia Bunge Maalum la Katiba leo, Ijumaa, Machi 21, 2014.
Muda
mfupi baada ya kuwa amewasili na kulakiwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda kwenye Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma, Rais Kikwete
ameendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri lake kwenye Ukumbi wa TAMISEMI
ikiwa ni shughuli yake ya kwanza katika ziara hiyo fupi ya Mkoa wa
Dodoma.
Leo,
Ijumaa, Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi na atahutubia Bunge Maalum la
Katiba kutokana na mwaliko wa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mheshimiwa
Samuel J. Sitta ambaye alimwalika Rais Kikwete kwa barua yake ya Machi
15, mwaka huu, ambayo ilijibiwa Machi 18, mwaka huu, kwa Rais Kikwete
kukubali mwaliko huo.
Mwaliko
huo wa Mheshimiwa Sitta kwa Rais Kikwete umetolewa kwa mujibu wa Kanuni
ya 7(1) (g) na Kanuni 75 (1) ya Kanuni za Bunge Maalum ambazo zinampa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum madaraka ya kumwalika Mgeni Rasmi aweze
kuhutubia Bunge Maalum.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
20 Machi, 2013
No comments:
Post a Comment