Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan
Kikwete akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo la hilo
kulia kwake ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na
Mbunge wa viti maalum wa jimbo la Charinze Subira Mgalu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya
kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu
fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.
Ridhwani achukua fomu za Ubunge Chalinze.
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete jana alichukua fomu katika ofisi za msimamizi wa
uchaguzi wilayani Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.
Akisindikizwa
na mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM wa jimbo la Chalinze na
Bagamoyo, Ridhwani alimhakikishia ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya
Bagamoyo Shija Andrew, kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na
kutoendesha kampeni za matusi na vurugu.
Baada
ya kuchukua fomu hiyo pamoja na nakala nyingine muhimu za uchaguzi
aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake kuelekea kwenye ofisi za CCM
Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa habari.
Katika
mazungumzo yake hayo Ridhwan alitaja vipaumbele vyake kwa kuleta
maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo alisisitizia kuimarisha
upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha afya, elimu pamoja
na kukuza ajira kwa vijana.
"Kama
mnavyofahamu kuwa Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na changamoto
nyingi kama vile maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa vijana sasa
pindi ambapo nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa napunguza
kama sio kumaliza kabisa tatizo hilo"alisema Ridhwan. Aliongeza
kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa
wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa
matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya
kushirikiana na wananchi kumaliza shida za Chalinze".
Ridhwan
pia alisema kuwa atasaidia kutatua ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba
wakulima na wafugaji na kuwataka wakazi wa Chalinze kumchagua kwa
kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa
tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua fomu
alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha
ya wakazi wa Chalinze.
Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.
No comments:
Post a Comment