
Nyama
nyekundu inaelezwa kuwa ni moja ya vyakula vinavyopunguza urefu wa maisha
.
Kwa miaka
mingi sana binadamu wa karne zote wamekuwa wakitafuta siri za maisha marefu,
kuzuia uzee na hata kuzuia kifo.
Lakini
pamoja na jitihada nyingi mambo haya yameendelea kuwa changamoto kubwa kwenye
maisha ya mwanadamu katika nchi mbalimbali duniani.
Kwa
Tanzania, inakadiriwa kuwa umri wa kuishi kwa wanaume ni takriban miaka 58.2 na
kwa wanawake ni miaka 60.5.
Muda huu
wa kuishi ni mfupi sana ikilinganishwa na wenzetu katika nchi zilizoendelea
kama vile Marekani ambako wastani wa kuishi ni unakadiriwa kuwa ni miaka 78.2.
Wanasayansi
wamekuwa na nadharia nyingi kuhusu sababu zinazosababisha binadamu azeeke na
kufa mapema. Ila wengi hufikiri kuwa tunazeeka mapema kutokana na sababu za
maumbile na vinasaba tunavyorithi kwa wazazi wetu.
Wengine
husema kuwa tunazeeka haraka kutokana na kuwa na mtindo usiofaa wa maisha.
Mtaalamu
wa Afya, Dk Mark Stibich anasema kwamba kuzeeka haraka na kuishi maishi
mafupi ni suala mtambuka na linahusisha mambo kama vile vinasaba, kemia,
fiziolojia ya mwili pamoja na tabia zetu kwa mujibu wa makala yake ya Mei
10, 2014 liyowekwa kwenye tovuti ya longevity.about.com.
Mtaalamu
wa maabara nchini Ujerumani, Dk James Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia
kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya
kuzeeka haraka hutokana na mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni.
Dk Vaupel
anaongeza kusema kuwa tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hata pacha wanaozaliwa
siku moja, hupishana urefu wa maisha kwa karibu miaka 10 kutokana na kuwa na
mitindo tofauti ya maisha.
Tafiti
nyingi zinaonyesha kuwa wakazi wa maeneo wanaoishi maisha marefu zaidi duniani
kama vile Japani, Italia na Marekani, pamoja na mambo mengine,
wanajiepusha na matumizi ya vileo, tumbaku na kupunguza ulaji wa nyama
nyekundu.
Pia huvuta
hewa safi ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi ngumu kila
siku.
Watu hawa pia huwa na mtazamo chanya
wa maisha, mazoezi na chakula asilia cha mimea kama vile mbogamboga na matunda
kwa wingi.
Vyakula vya
asili vineelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa matokeo ya watu kuishi miaka
mingi kuliko wale ambao hawazingatii utaratibu huo.
Katika
utafiti mmoja uliofanyika huko Japan, iligundulika kuwa chakula chenye
asili ya mimea kinaongeza ubora na urefu wa maisha.
Katika
utafiti huo, wanawake vikongwe 200 walioshiriki katika utafiti walithibitika
kuwa katika kipindi cha juma moja, hutumia zaidi ya aina 100 za vyakula vyenye
asili ya mimea.
Jambo
lingine likaonekana kwamba wamekuwa wakifanya hivyo kwa kipindi kirefu cha
maisha yao. Ripoti hii ni kwa mujibu wa Cook, G.C na Zumla A katika kitabu chao
cha Manson’s Tropical Diseases, toleo la 21.
Katika
utafiti wa Dk Pan A na wenzake uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archives
of Internal Medicine, la Machi, 2012, inaonekana kuwa kula nyama nyekundu
kwa wingi, hupunguza umri wa kuishi.
Nyama
yenye shida kubwa ni ile yenye mafuta mengi, nyama choma iliyoungua na ile
iliyosindikwa.
Nyama ya
namna hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na
saratani ya utumbo.
Hii
inasababishwa na uzalishaji wa kemikali kama n-nitrosa na polycyclic
aromatic hydrocarbons (PAHs) zinazodhuru afya.
Ingawa
jamii ya Wamasai wanakula nyama nyekundu kwa wingi, tafiti zinaonyesha kuwa
wanatumia pia mitishamba (acacia goetzei na albizia anthelmintica).
Pia
hutumia vyakula vya mimea kwa wingi vikiwa katika uasilia wake, jambo ambalo
huwapunguzia hatari itokanayo na nyama.
Hilo ni
kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Johns T na wenzake walioufanya Ngorongoro
mwaka 1999 na kuchapishwa katika jarida la dawa za asili lijulikanalo kama J.
Ethnopharmacology.
Katika utafiti mwingine uliofanywa
na Dk Dean Ornish na madaktari wenzake wa Chuo Kikuu cha Califonia na San
Francisco (UCSF), iligundulika kuwa mazoezi na mtindo bora wa maisha huimarisha
afya ya vinasaba vya mwili vinavyohusika na kuzeeka vijulikanavyo kama telomeres.
Mazoezi
yanaelezewa kuwa hufanya telomeres virefuke, hivyo kuongeza maisha. Telomeres
zinapoathirika na kuwa fupi husababisha seli za mwili kudhurika na maisha kuwa
mafupi.
Utafiti
huu ulichapishwa kwenye jarida la The Lancet Oncology la Septemba, 2013.
Jambo
jingine linalochangia kuwa na maisha marefu, ni uhusiano mzuri katika familia
na jamii, kwa mujibu wa utafiti wa Rikke Lund wa Chuo Kikuu cha Copenhagen
Denmark na wenzake katika jarida la Epidemiolojia na afya ya jamii mwaka
2014.
Wataalamu
wengine wa masuala ya afya ya jamii wanaongeza kusema kuwa, uhusiano bora na
mtazamo chanya katika maisha huongeza urefu wa maisha kwa miaka saba na nusu.
Katika
utafiti mwingine uliochapishwa katika jarida la tiba la Uingereza la British
Medical, watafiti pia waligundua kuwa kutoelewana, ugomvi na mabishano ya
mara kwa mara ya wanafamilia au wanandoa, huchangia watu kufa mapema zaidi.
Taarifa
hii ilichapishwa katika mtandao wa kisayansi wa Science Daily la Mei 8,
mwaka huu.
Kutokana
na maelezo ya tafiti hizo, unaweza kubaini kuwa kuishi maisha marefu duniani,
kunaweza kutegemea mfumo wa maisha wa mtu pamoja na mazingira yake.
Ukizingatia
baadhi ya kanuni hizo za kitaalamu unaweza kuishi muda mrefu duniani.
Clifford
Majani ni mmoja wa watafiti, Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Mbeya
(NIMR-MMRC)
anuni za sayansi za kusaidia mtu kuishi maisha marefu

Nyama nyekundu inaelezwa kuwa ni moja ya vyakula vinavyopunguza urefu wa maisha
.
Kwa miaka mingi sana binadamu wa karne zote wamekuwa wakitafuta siri za maisha marefu, kuzuia uzee na hata kuzuia kifo.
Lakini pamoja na jitihada nyingi mambo haya
yameendelea kuwa changamoto kubwa kwenye maisha ya mwanadamu katika nchi
mbalimbali duniani.
Kwa Tanzania, inakadiriwa kuwa umri wa kuishi kwa wanaume ni takriban miaka 58.2 na kwa wanawake ni miaka 60.5.
Muda huu wa kuishi ni mfupi sana ikilinganishwa na
wenzetu katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako wastani wa
kuishi ni unakadiriwa kuwa ni miaka 78.2.
Wanasayansi wamekuwa na nadharia nyingi kuhusu
sababu zinazosababisha binadamu azeeke na kufa mapema. Ila wengi
hufikiri kuwa tunazeeka mapema kutokana na sababu za maumbile na
vinasaba tunavyorithi kwa wazazi wetu.
Wengine husema kuwa tunazeeka haraka kutokana na kuwa na mtindo usiofaa wa maisha.
Mtaalamu wa Afya, Dk Mark Stibich anasema kwamba
kuzeeka haraka na kuishi maishi mafupi ni suala mtambuka na linahusisha
mambo kama vile vinasaba, kemia, fiziolojia ya mwili pamoja na tabia zetu kwa mujibu wa makala yake ya Mei 10, 2014 liyowekwa kwenye tovuti ya longevity.about.com.
Mtaalamu wa maabara nchini Ujerumani, Dk James
Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu
pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya kuzeeka haraka hutokana na
mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni.
Dk Vaupel anaongeza kusema kuwa tafiti nyingi
zinaonyesha kuwa hata pacha wanaozaliwa siku moja, hupishana urefu wa
maisha kwa karibu miaka 10 kutokana na kuwa na mitindo tofauti ya
maisha.
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wakazi wa maeneo
wanaoishi maisha marefu zaidi duniani kama vile Japani, Italia na
Marekani, pamoja na mambo mengine, wanajiepusha na matumizi ya vileo,
tumbaku na kupunguza ulaji wa nyama nyekundu.
Pia huvuta hewa safi ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi ngumu kila siku.
Watu hawa pia huwa na mtazamo chanya wa maisha, mazoezi na chakula asilia cha mimea kama vile mbogamboga na matunda kwa wingi.
Vyakula vya asili vineelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa
matokeo ya watu kuishi miaka mingi kuliko wale ambao hawazingatii
utaratibu huo.
Katika utafiti mmoja uliofanyika huko Japan,
iligundulika kuwa chakula chenye asili ya mimea kinaongeza ubora na
urefu wa maisha.
Katika utafiti huo, wanawake vikongwe 200
walioshiriki katika utafiti walithibitika kuwa katika kipindi cha juma
moja, hutumia zaidi ya aina 100 za vyakula vyenye asili ya mimea.
Jambo lingine likaonekana kwamba wamekuwa
wakifanya hivyo kwa kipindi kirefu cha maisha yao. Ripoti hii ni kwa
mujibu wa Cook, G.C na Zumla A katika kitabu chao cha Manson’s Tropical Diseases, toleo la 21.
Katika utafiti wa Dk Pan A na wenzake uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archives of Internal Medicine, la Machi, 2012, inaonekana kuwa kula nyama nyekundu kwa wingi, hupunguza umri wa kuishi.
Nyama yenye shida kubwa ni ile yenye mafuta mengi, nyama choma iliyoungua na ile iliyosindikwa.
Nyama ya namna hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na saratani ya utumbo.
Hii inasababishwa na uzalishaji wa kemikali kama n-nitrosa na polycyclic aromatic hydrocarbons (PAHs) zinazodhuru afya.
Ingawa jamii ya Wamasai wanakula nyama nyekundu kwa wingi, tafiti zinaonyesha kuwa wanatumia pia mitishamba (acacia goetzei na albizia anthelmintica).
Pia hutumia vyakula vya mimea kwa wingi vikiwa katika uasilia wake, jambo ambalo huwapunguzia hatari itokanayo na nyama.
Hilo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Johns T
na wenzake walioufanya Ngorongoro mwaka 1999 na kuchapishwa katika
jarida la dawa za asili lijulikanalo kama J. Ethnopharmacology.
Katika utafiti mwingine uliofanywa na Dk Dean
Ornish na madaktari wenzake wa Chuo Kikuu cha Califonia na San Francisco
(UCSF), iligundulika kuwa mazoezi na mtindo bora wa maisha huimarisha
afya ya vinasaba vya mwili vinavyohusika na kuzeeka vijulikanavyo kama telomeres.
Mazoezi yanaelezewa kuwa hufanya telomeres virefuke, hivyo kuongeza maisha. Telomeres zinapoathirika na kuwa fupi husababisha seli za mwili kudhurika na maisha kuwa mafupi.
Utafiti huu ulichapishwa kwenye jarida la The Lancet Oncology la Septemba, 2013.
Jambo jingine linalochangia kuwa na maisha marefu,
ni uhusiano mzuri katika familia na jamii, kwa mujibu wa utafiti wa
Rikke Lund wa Chuo Kikuu cha Copenhagen Denmark na wenzake katika jarida
la Epidemiolojia na afya ya jamii mwaka 2014.
Wataalamu wengine wa masuala ya afya ya jamii
wanaongeza kusema kuwa, uhusiano bora na mtazamo chanya katika maisha
huongeza urefu wa maisha kwa miaka saba na nusu.
Katika utafiti mwingine uliochapishwa katika jarida la tiba la Uingereza la British Medical,
watafiti pia waligundua kuwa kutoelewana, ugomvi na mabishano ya mara
kwa mara ya wanafamilia au wanandoa, huchangia watu kufa mapema zaidi.
Taarifa hii ilichapishwa katika mtandao wa kisayansi wa Science Daily la Mei 8, mwaka huu.
Kutokana na maelezo ya tafiti hizo, unaweza
kubaini kuwa kuishi maisha marefu duniani, kunaweza kutegemea mfumo wa
maisha wa mtu pamoja na mazingira yake.
Ukizingatia baadhi ya kanuni hizo za kitaalamu unaweza kuishi muda mrefu duniani.
Clifford Majani ni mmoja wa watafiti, Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Mbeya (NIMR-MMRC)
No comments:
Post a Comment