SEVILLA
ya Hispania imetwaa ubingwa wa Europa League baada ya kuifunga Benfica
ya Ureno kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika
120.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata mashambulizi yawe machache
Bacca,
M’Bia, Coke na Gameiro ndiyo walifunga penalti za Sevilla, wakati wa
Cardozo na Rodrigo walikosa za Benfica, huku Lima na Luisao wakifunga.
Sifa
zimuendee kipa Mreno wa Sevilla Antonio Alberto Bastos Pimparel
aliyewazuilia ndugu zake leo na kucheza penalti moja ya Rodrigo, wakati
ya Cardozo ilikwenda nje.
Ushindi
wa Sevilla unamaanisha mataji yote ya klabu ya UEFA msimu huu yamebaki
Hispania, kwani Atletico Madrid na Real Madrid nazo zitakutana katika
Fainali ya Ligi ya Mabingwa baadaye mwezi huu nchini Ureno.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata mashambulizi yawe machache

Vikosi vilikuwa, Sevilla:
Beto, Coke, Pareja, Fazio, Moreno, Mbia, Carrico,
Reyes/Marin dk78/Gameiro dk104, Rakitic, Vitolo/Diogo Figueiras dk110 na
Bacca.
Benfica:
Oblak, Maxi Pereira, Luisao, Garay, Siqueira/Cardozo dk99, Ruben
Amorim, Gomes, Gaitan/Ivan Calvaleiro dk119, Sulejmani/Andre Almeida
dk25, Lima na Rodrigo.
Tukio lingine lililo make head line jana ni KIUNGO
Ivan Rakitic alikuwa nyota usiku wa jana wakati Seville ikiifunga
Benfica kwa penalti na kutwaa taji la Europa League mjini Turin.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Croatia alicheza soka ya kiwango cha nyota wa
mchezo na kisha akamalizia kwa kunyonyana mdimi na beki wa zamani wa
Reading, Daniel Carrico.
Rakitic amekuwa mmoja wa viungo bora barani Ulaya kwa sasa kiasi cha timu kibao barani humo sass kuanza kuisaka huduma yake.

Taji: Rakitic akiwa amepozi na taji Europa League usiku wa kuamkia leo baada ya Sevilla kuifunga Benfica kwa penalti.
No comments:
Post a Comment