MSHAMBULIAJI
mtukutu, Super Mario Balotelli macho yake hayakuwa kwa taifa lake tu,
bali hata kwa mchumba wake Fanny Neguesha ambaye alikuwa miongoni mwa
mashabiki waliofurika katika mchezo wa ufunguzi wa Italia wa kundi D
dhidi ya Simba watatu, timu ya taifa ya Engaland.
Katika
mechi hiyo ambayo Balotelli aliifungia Italia bao katika ushindi wa
2-1, mchuchu wa nyota huyo alivalia jezi namba 9 ya Italia yenye jina la
basha wake, Balotelli.
Neguesha
kwa muda wote alikuwa na tabasamu baada ya mpenzi wake kufunga bao safi
kwa kichwa mapema kipindi cha pili na kuifanya Italia iwe mbele kwa
mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment